Mwandishi: Suleiman Ali

  • Marekani Yakasirishwa na Uchaguzi wa Iran katika Uongozi wa Mkutano wa Nyuklia

    Marekani Yakasirishwa na Uchaguzi wa Iran katika Uongozi wa Mkutano wa Nyuklia

    Marekani imeonyesha hasira kufuatia kuchaguliwa kwa Iran kuwa miongoni mwa wajumbe wa meza ya uratibu ya Mkutano wa Mapitio ya Mkataba wa Kutokomeza Silaha za Nyuklia, hatua iliyokuja licha ya juhudi za Washington kuzuia uteuzi huo.w

    Katika kikao hicho, mwakilishi wa Marekani aliingia kwenye malumbano ya maneno na mwakilishi wa Iran, akieleza kuwa serikali ya Rais Donald Trump imeshangazwa na kuchukizwa sana na uamuzi wa kumchagua Iran kushika nafasi hiyo ya uongozi katika mkutano huo wa kimataifa.

  • Kansela wa Ujerumani: Wairani ni wazi kuwa wana nguvu zaidi kuliko ilivyodhaniwa

    Kansela wa Ujerumani: Wairani ni wazi kuwa wana nguvu zaidi kuliko ilivyodhaniwa

    Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz, amesema kuwa Iran inaonyesha kuwa na uwezo na nguvu kubwa kuliko inavyokadiriwa mara nyingi na jamii ya kimataifa. Kauli hiyo ilitolewa katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya.Merz alisema kuwa katika mazungumzo yanayoendelea kati ya Marekani na Iran, chini ya usuluhishi wa Pakistan, hakuna nchi iliyoonyesha upinzani kuhusu uwezekano wa kupunguza vikwazo dhidi ya Iran endapo Tehran itaonyesha utayari wa kutoa masharti au ustahiki unaotakiwa katika mazungumzo hayo.Aidha, Kansela huyo alieleza kuwa suala la kupunguza vikwazo kwa utaratibu wa hatua kwa hatua limejadiliwa kama sehemu ya mpango wa masharti maalum unaoweza kutumika iwapo pande husika zitafikia makubaliano.

  • Sheikh Naim: Iran, Mhusika Muhimu Katika Kusitishwa kwa Mapigano Lebanon

    Sheikh Naim: Iran, Mhusika Muhimu Katika Kusitishwa kwa Mapigano Lebanon

    Katibu Mkuu wa Hezb nchini Lebanon, Sheikh Naim Qassem, amesema kuwa usitishwaji wa mapigano nchini humo usingewezekana bila ushiriki wa Iran katika mazungumzo yaliyofanyika nchini Pakistan. Akizungumza kuhusu mchango wa Iran katika jitihada za amani, Sheikh Qassem alisema kuwa “kama Jamhuri ya Kiislamu ya Iran isingekuwepo katika mazungumzo hayo, baada ya ushujaa na uvumilivu wa wananchi na wapiganaji wa Lebanon, kusingepatikana makubaliano ya kusitisha vita.” Aliongeza kuwa serikali ya Lebanon haikupaswa kuchukua msimamo wa hasira dhidi ya hatua ya kusitisha vita, akisisitiza kwamba “hakuna mamlaka yoyote nje ya Lebanon yenye haki ya kuweka masharti kwa nchi hii.” Kuhusu mashambulizi yaliyojulikana kama “Jumatano Nyeusi”, Sheikh Qassem alibainisha kuwa adui alifanya mashambulizi zaidi ya 200 ndani ya dakika 10 na kusababisha vifo vya mamia ya raia wasiokuwa na hatia, kisha kudai kuwa serikali ya Lebanon haina dhamira ya kusitisha mapigano. Aidha, alikosoa hatua ya serikali kukutana moja kwa moja na maofisa wa Marekani mjini Washington, akisema siku hiyo ilikuwa “ya fedheha kwa taifa.” Qassem alisema makubaliano yaliyopatikana yalikuwa ya upande mmoja, yakiiwezesha Israel kuendelea na mashambulizi yake huku yakilipachika kundi la wapiganaji wanaolinda Lebanon jina la “waasi”. Sheikh Qassem alihitimisha kwa kuuliza, “Je, serikali ya Lebanon inasimama upande wa adui?”

  • Putin: Nimepokea ujumbe kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Iran

    Putin: Nimepokea ujumbe kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Iran

    Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa alipokea ujumbe kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wiki iliyopita.Putin pia alimtakia Kiongozi Mkuu wa Iran afya njema na mafanikio, akisisitiza kuwa anatumai salamu zake za dhati zitawasilishwa kwake.Aidha, rais huyo wa Urusi alieleza kuwa nchi yake iko tayari kufanya juhudi zozote zitakazolinda maslahi ya Iran pamoja na nchi nyingine za eneo hilo, kwa lengo la kusaidia kurejesha amani katika Mashariki ya Kati kwa haraka iwezekanavyo.

  • Netanyahu akemewa mtandaoni baada ya kulaani jaribio la mauaji ya Trump

    Netanyahu akemewa mtandaoni baada ya kulaani jaribio la mauaji ya Trump

    Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amejikuta katika wimbi zito la ukosoaji kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kauli yake ya kulaani matumizi ya nguvu, muda mfupi baada ya jaribio la kumuua Rais wa Marekani, Donald Trump. Katika taarifa yake, Netanyahu alisema wazi kuwa, “Hakuna nafasi ya ghasia; si dhidi ya viongozi wa kisiasa, wala dhidi ya mtu mwingine yeyote.” Hata hivyo, kauli hiyo imepokelewa kwa hisia mseto, huku makala moja ikimwelezea kwa maneno makali na kumuita “Gaidi analiyeua watoto wengi zaidi duniani.” Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wametumia fursa hiyo kukosoa na kudhihaki matamshi hayo, wakikumbusha operesheni za jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza na tuhuma za mauaji ya viongozi mbalimbali wa Iran, Palestina, na Lebanon.

  • Kenya na Uganda Kuwekeza Tanzania

    Kenya na Uganda Kuwekeza Tanzania

    Kenya na Uganda ziko kwenye mazungumzo ya kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Tanzania ili kupunguza utegemezi wa bidhaa za petroli zinazoagizwa kutoka nje, na kuhudumia nchi zinazozalisha mafuta ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).