Kategoria: KIMATAIFA

  • Trump “amechoshwa” na amekasirishwa na vita vya Iran

    Trump “amechoshwa” na amekasirishwa na vita vya Iran

    Trump anaripotiwa kuchoshwa na kukatishwa tamaa na vita dhidi ya Iran, huku mzozo huo ukiendelea kwa muda mrefu zaidi kuliko alivyotarajia na bila dalili ya ushindi wa wazi. Kulingana na taarifa hiyo, Trump angependa kuelekeza tena umakini wake kwenye masuala mengine, ikiwemo siasa za ndani za Marekani, mazungumzo ya biashara na China, pamoja na vipaumbele vingine vya sera.

    Hata hivyo, Iran inaendelea kupinga mazungumzo na hivyo kurefusha mzozo huo.

    Chanzo: The Atlantic

  • Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Iran sasa ina nguvu ya kushinikiza

    Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Iran sasa ina nguvu ya kushinikiza

    Antony Blinken, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, amesema kuwa hali ya sasa inaonyesha kuwa Iran imepata nafasi ya kutumia nguvu ya ushawishi katika mwelekeo wa mazungumzo na hatua zinazoweza kufuata.

    wKwa mujibu wa Blinken, Donald Trump anatafuta njia ya kujinasua, huku akieleza matumaini yake kwamba makubaliano yatafikiwa.

    Aidha, aliongeza kuwa Iran sasa inashikilia nyenzo ya shinikizo na inatarajiwa kuitumia kwa manufaa yake katika hatua zijazo.

  • Rais Pezeshkian Amemsifia Kiongozi Muadhamu baada ya kukutana naye kwa muda wa masaa 2

    Rais Pezeshkian Amemsifia Kiongozi Muadhamu baada ya kukutana naye kwa muda wa masaa 2

    Rais Masoud Pezeshkian amesimulia kwa kina mkutano wake wa hivi karibuni na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Mojtaba Khamenei, akielezea hali ya kikao hicho pamoja na sifa za binafsi, kimaadili na kiuongozi alizozishuhudia kwa Kiongozi huyo.

    Rais Pezeshkian amesema mkutano huo ulifanyika katika mazingira ya ukarimu na uaminifu na kuendelea kwa takriban masaa mawili na nusu.

    Kwa mujibu wa Rais Pezeshkian, kilichojitokeza zaidi kuliko jambo lolote ni mtazamo wa unyenyekevu, uaminifu wa dhati na heshima ya hali ya juu wa Kiongozi Muadhamu, mwenendo uliogeuza kikao hicho kuwa majadiliano yaliyojengwa juu ya imani, utulivu, kuelewana na mazungumzo ya wazi ya moja kwa moja.

    Rais Pezeshkian amesisitiza pia umuhimu wa kuimarisha mshikamano, kuaminiana na huruma katika ngazi zote za usimamizi wa serikali na utawala wa nchi.

    Amebainisha kuwa pale kiongozi wa juu kabisa wa taifa anaposhirikiana na maafisa na wananchi kwa maadili ya hali ya juu, unyenyekevu na roho ya kuwajali watu, mwenendo huo huwa mfano wa kuigwa katika mfumo mzima wa utawala na uongozi wa nchi.

  • Urusi na China kupinga azimio la Marekani la Hormuz dhidi ya Iran katika umoja wa mataifa

    Urusi na China kupinga azimio la Marekani la Hormuz dhidi ya Iran katika umoja wa mataifa

    Urusi na China zinatarajiwa kupiga kura ya turufu dhidi ya rasimu ya azimio lililowasilishwa na Bahrain na Marekani kuhusu hali ya usalama katika Mlango wa Hormuz, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya kimataifa.

    WMtandao wa Al Jazeera umearifu kuwa hadi sasa Moscow na Beijing hawajawasilisha mapendekezo yoyote ya marekebisho kwa rasimu hiyo.Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa rasimu iliyowasilishwa na Marekani na Bahrain inaonekana kufanana kwa kiasi kikubwa na ile ambayo awali ilikataliwa na Urusi na China.

  • CBS: Mashambulizi mapya dhidi ya meli za kivita za Marekani yalikuwa makali zaidi kuliko yale ya siku chache zilizopita

    CBS: Mashambulizi mapya dhidi ya meli za kivita za Marekani yalikuwa makali zaidi kuliko yale ya siku chache zilizopita

    Washington, Marekani — Vyanzo vya shirika la habari la CBS vimeripoti kuwa meli za kivita za Marekani, USS Truxtun na USS Mason, zimeshambuliwa vikali na vikosi vya Iran katika Bahari ya Oman.

    Maafisa wa Marekani wameeleza kuwa mashambulizi hayo yalikuwa makubwa na ya muda mrefu zaidi ikilinganishwa na yale yaliyotekea siku kadhaa zilizopita.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, boti za kasi za Iran zilikaribia manowari hizo kwa umbali hatari, hali iliyozilazimisha meli za Marekani kutumia mizinga ya baharini, mfumo wa silaha za kujihami za karibu (CIWS) pamoja na bunduki zilizowekwa juu ya staha.

    AAidha, maafisa wa Marekani wamesema kuwa Iran ilitumia ndege zisizo na rubani (drones) na makombora katika oparesheni hiyo, jambo lililoonyesha ongezeko la uhasama na hatari katika eneo la ghuba.

  • Ufaransa: “Tunalipa gharama ya vita ambavyo hatukuvichagua”

    Ufaransa: “Tunalipa gharama ya vita ambavyo hatukuvichagua”

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa ameonya kuwa uwezekano wa kuondoa vikwazo dhidi ya Iran haupo kabisa hadi pale Mlango wa Hormuz utakapofunguliwa, akibainisha msimamo mkali wa Paris kuhusu hali inayoendelea katika eneo la Asia ya Magharibi.
    Akizungumza leo kwenye mahojiano maalum na kituo cha redio na televisheni cha RTL, waziri huyo aliweka wazi misimamo miwili mikuu: Kwanza, kusisitiza kuwa hatua yoyote ya kuondoa vikwazo haitazingatiwa wakati njia muhimu ya kimkakati kama Hormuz ipo katika hali ya kuzuiwa.
    wPili, aliitaka Ulaya kuelekeza nguvu zaidi katika kupunguza utegemezi ambao, kwa maneno yake, “umeilazimisha kulipia gharama za vita ambavyo si chaguo lake.”Katika mahojiano hayo yaliyofanyika saa chache kabla ya kutolewa kwa jibu la Iran kuhusu pendekezo la amani la Marekani, waziri alisema Iran—inayodai kuhitaji kuondolewa kwa vikwazo kama sehemu ya makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia—haiwezi kutarajia hatua hiyo huku hali ya usalama katika Mlango wa Hormuz ikiwa bado tete.