Kategoria: UCHAMBUZI

  • Hasara ya kila wiki ya dola milioni 60 kwa kampuni ya Kijerumani kutokana na mgogoro wa Hormuz

    Hasara ya kila wiki ya dola milioni 60 kwa kampuni ya Kijerumani kutokana na mgogoro wa Hormuz

    Kampuni ya Kijerumani yapata hasara ya dola milioni 60 kwa wiki kutokana na mgogoro wa Hormuz

    🔹Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya usafirishaji ya Kijerumani, Hapag-Lloyd, amesema kuwa kuendelea kwa mgogoro katika Mlango wa Hormuz kumeisababishia kampuni hiyo gharama za ziada za kati ya dola milioni 50 hadi 60 kila wiki.

    🔹Ameongeza kuwa hata kama mvutano utapungua, sekta ya usafiri wa baharini itahitaji wiki kadhaa kurejea kikamilifu katika hali ya kawaida.

  • Ghana yakataa dili nono ya Amerika kutokana na hitaji la kufichua data za raia

    Ghana yakataa dili nono ya Amerika kutokana na hitaji la kufichua data za raia

    Utawala wa Rais John Dramani Mahama ulikataa mpango ambapo uliihitaji kupata msaada wa kifedha kwa kuipa Amerika data yake muhimu ya kiafya.Suala hilo hilo lilizima mazungumzo kati ya Amerika na Zimbabwe na pia mahakama ya Kenya ilizima mkataba kama huo baada ya kesi kuwasilishwa na Shirika moja la kiraia.Msemaji wa serikali ya kigeni ya Ghana na serikali haikujibu jumbe za Reuters kuhusu suala hilo. Amerika nayo ilisema kuwa huwa haifichui maelezo kuhusu mikataba yake ya kibiashara na mataifa mengine.“Tunaendelea kuangalia njia ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili,” msemaji wa serikali akasema.Mnamo Septemba, utawala wa Amerika ulitangaza mbinu mpya ya kiulimwengu ambayo ni ya kuhakikisha mataifa maskini yanatelekeza wajibu katika kupambana na ukimwi, malaria, pumu, polio nchini mwao.Hii ilikuwa mbinu ya kuyazuia mataifa hayo kutegemea msaada wa Amerika na kujitegemea.Mamlaka ya Kimataifa ya Maendeleo Amerika ilivunjwa mapema mwaka huu.Amerika ilikuwa imetuma Sh28.3 milioni kama msaada kwa Ghana ikiwemo Sh12.4 bilioni kwa sekta ya afya 2024, kabla ya Rais Donald Trump kuyapunguza msaada kwa nchi za kigeni.

  • Putin: Kuendelea kwa vita kati ya Marekani na Iran hakuna faida kwa yeyote

    Putin: Kuendelea kwa vita kati ya Marekani na Iran hakuna faida kwa yeyote

    Putin amesema kuwa kuendelea kwa vita kati ya Marekani na Iran hakutanufaisha upande wowote.

    Amesema pia kuwa mgogoro huo ni mgumu sana na umeiweka Urusi katika hali ngumu, akieleza kwamba Moscow ina uhusiano mzuri na Iran pamoja na nchi za Kiarabu.

  • Hormuz : Mshipa Mkuu wa Intaneti ya Dunia

    Hormuz : Mshipa Mkuu wa Intaneti ya Dunia

    Mlango wa Bahari wa Hormuz, unaojulikana duniani kama njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta, una jukumu jingine nyeti ambalo mara chache huzungumziwa: kuwa sehemu ya moja ya njia kuu za miundombinu ya intaneti ya kimataifa.

    Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, zaidi ya nyaya kadhaa za nyuzi za macho zilizowekwa chini ya bahari—zinazounganisha bara la Asia, Ulaya na eneo la Mashariki ya Kati—hupitia katika sehemu hii nyeti ya kijiografia. Nyaya hizi ni kiungo muhimu kwa huduma za kimataifa za mawasiliano, ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa data, mifumo ya wingu, miamala ya kifedha na huduma nyingine za kidijitali.

    Wataalamu wanaonya kuwa hitilafu au uharibifu wowote katika nyaya hizi unaweza kusababisha athari kubwa kwa upatikanaji wa intaneti katika mataifa mengi, jambo ambalo linaweza kuathiri vibaya uchumi wa kidijitali na shughuli za kibiashara za kimataifa.

    Katika siku za karibuni, suala hili limepata uangalizi mpana kutoka kwa vyombo vya habari vya kimataifa. Ripoti nyingi—hasa kutoka vyombo vya habari vya India—zimeangazia umuhimu wa kimkakati wa eneo hilo na hatari zinazoweza kutokea endapo miundombinu hiyo itapatwa na dosari.

  • Beijing: China Yasema Inawasiliana na Iran Kupunguza Mvutano

    Beijing: China Yasema Inawasiliana na Iran Kupunguza Mvutano

    Beijing — China imesema inaendelea kuwasiliana na pande zote husika, ikiwemo Iran, katika juhudi za kupunguza mvutano na kumaliza mapigano yanayoendelea katika eneo hilo.Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema kuwa Beijing inaweka wazi njia za mawasiliano na wadau wote kwa lengo la kusaidia kupunguza hali ya taharuki na kuhimiza mwisho wa mzozo.China pia imesisitiza kuwa inaunga mkono ushirikiano wa kiusalama pamoja na kuendelezwa kwa mazungumzo ya amani katika Mashariki ya Kati.Kwa mujibu wa msemaji huyo, raia wa China walikuwemo katika meli ya mafuta iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Visiwa vya Marshall, ambayo ilishambuliwa katika Mlango wa Hormuz, lakini hakuna aliyepata majeraha.Aidha, China imeeleza wasiwasi wake kuhusu kukamatwa kwa meli kadhaa katika eneo hilo, na kuzitaka pande zote kuhakikisha usafiri wa kawaida wa majini unapitia tena kwa usalama katika Mlango wa Hormuz.Beijing imesema kuwa kurejeshwa kwa usafiri wa majini usio na vikwazo kupitia Mlango wa Hormuz ni kwa manufaa ya nchi za eneo hilo pamoja na jumuiya ya kimataifa.

  • Iran yaharibu mpango wa Trump kuhusu Kombe la Dunia

    Iran yaharibu mpango wa Trump kuhusu Kombe la Dunia

    Iran imevuruga mipango ya Rais wa Marekani, Donald Trump, si tu katika nyanja za uchumi, siasa na masuala ya kijeshi kufuatia mvutano kati ya pande hizo mbili, bali pia katika mradi unaohusiana na Kombe la Dunia FIFA 2026.Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa Jumanne na jarida la The Athletic, mpango wa Trump wa kufanikisha mapato ya takriban dola bilioni 30 kupitia Kombe la Dunia umekumbwa na changamoto, baada ya wamiliki wa hoteli katika miji 11 itakayokuwa wenyeji wa mashindano hayo kuripoti kushuka maombi kwa asilimia 60 chini ya matarajio.Ripoti zinasema kuwa karibu asilimia 70 ya mapato yanayotarajiwa na Marekani kutokana na Kombe la Dunia yanatokana na sekta ya utalii, hasa kupitia mashabiki wanaosafiri kuhudhuria mechi na kutumia huduma za hoteli. Takwimu zilizotolewa na wamiliki wa hoteli zinaonyesha kuwa sehemu kubwa ya malengo hayo haijafikiwa.Ripoti zinaeleza kuwa hapo awali Trump alifanya mikutano kadhaa ya kutangaza mashindano hayo pamoja na Rais wa FIFA, Gianni Infantino, akilenga kuonyesha kuwa kungekuwako mwitikio mkubwa wa kimataifa.Hata hivyo, kadiri muda wa kuanza mashindano ya Kombe la Dunia unavyokaribia, takwimu zinaonyesha kuwa mwitikio wa mashabiki ni mdogo kuliko ilivyotarajiwa.Gazeti la Mirror la Uingereza limeripoti kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia kupungua idadi ya wasafiri kwenda Marekani kuhudhuria mashindano ya Kombe la Dunia ni sera za kuchochea vita za Trump, ambazo zimevuruga hali ya Mashariki ya Kati na maeneo mengine duniani.Aidha, gazeti hilo limetaja sababu nyingine zinazochangia hoteli kubaki na vyumba tupu kuwa ni kupanda bei za tiketi za mechi hadi mara sita zaidi ikilinganishwa na Kombe la Dunia la Qatar, ongezeko la ada za maegesho ya magari hadi mara nne, pamoja na sera kali za utumiaji mabavu za polisi zinazotekelezwa dhidi ya wahamiaji na baadhi ya wasafiri.