Kategoria: Uncategorized

  • Trump: Si lazima kuchukua ‘vumbi la nyuklia’ la Iran

    Trump: Si lazima kuchukua ‘vumbi la nyuklia’ la Iran

    Trump asema kuchukua nyenzo za nyuklia za Iran si jambo la lazima

    🔹Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa kuchukua nyenzo za nyuklia za Iran si lazima. Kauli hiyo aliitoa katika mahojiano aliyofanya usiku uliopita na kituo cha habari cha Fox News.

    🔹Katika mahojiano hayo, Trump alieleza mawazo mbalimbali, baadhi yake yakionekana kutofautiana, kuhusu suala la kuchukuliwa kwa urani iliyorutubishwa ya Iran—ambayo wakati mwingine huirejelea kwa jina la “vumbi la nyuklia”.

  • Kenya yaomba kiti cha kudumu kwenye Baraza la UN

    Kenya yaomba kiti cha kudumu kwenye Baraza la UN

    Rais wa Kenya, William Ruto, ametoa wito kwa Afrika kupewa uanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, takwa ambalo limeungwa mkono na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.Rais William Ruto ametoa wito huo katika mkutano wa kilele wa Afrika na Ufaransa unaofanyika jijini Nairobi.Ruto amesema: “Afrika inapaswa kuwa na mwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,” na ni wakati wa Umoja wa Mataifa kutambua bila kuchelewa kwamba Afrika haipaswi kukabiliwa na maamuzi ambayo haishirikishwi kuyachukuwa. Rais Ruto amesema ukosefu wa haki unaoshuhudiwa katika mfumo wa kimataifa unaimarisha mgawanyiko, na ametoa wito wa kufanyika mageuzi ya mfumo wa kitaasisi wa Umoja wa Mataifa kama haja ya kimkakati.Rais wa Kenya amesisitiza kwamba Afrika inataka kuondokana na utegemezi, kuwa na nafasi kubwa na kuwa mshirika kamili katika ngazi ya soko, kutokana na kuwa na kundi kubwa la vijana watanashati.Pia ametoa wito kwa nchi za Afrika kuhimiza uwekezaji wa kitaifa na ushirikiano wa kimkakati wa kimataifa, na akasema ni muhimu kwa Afrika kurekebisha mifumo yake, kwa sababu Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa pekee haziwezi kutimiza malengo ya ustawi katika bara hilo.Viongozi kutoka nchi zaidi ya 30 akiwemo Rais Emannuel Macron wa Ufaransa wanashiriiki katika mkutano wa Nairobi unaojadili amani na usalama, kuimarisha uwekezaji endelevu, kurekebisha mfumo wa fedha wa kimataifa, pamoja na mabadiliko katika sekta ya nishati na kuunganisha vipaumbele vya Afrika ndani ya mifumo ya uchumi wa dunia.Mkutano huo pia unachunguza njia za kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Afrika na Ufaransa, pamoja na kushughulikia changamoto zinazohusiana na ustawi, mabadiliko ya kidijitali, na mada zingine.Mkutano wa kilele wa Ufaransa na Afrika unafanyika katika kivuli cha changamoto kubwa zinazoikabili Ulaya, zinazotokana na vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran na athari zake ambazo zimeathiri dunia nzima.

  • China yawahukumu kifo mawaziri wawili wa zamani wa ulinzi

    China yawahukumu kifo mawaziri wawili wa zamani wa ulinzi

    Beijing — Katika hatua ya kushangaza huku kukiendelea msako ndani ya jeshi lake, China siku ya Alhamisi iliwapa mawaziri wake wawili wa zamani wa ulinzi adhabu ya kifo iliyoahirishwa kwa tuhuma za ufisadi.

    Wei Fenghe na Li Shangfu wote walipatikana na hatia ya kupokea rushwa na wakahukumiwa adhabu ya kifo yenye kusitishwa kwa miaka miwili na mahakama ya kijeshi ya nchi hiyo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.

    Mahakama ilitangaza kuwa baada ya miaka miwili, adhabu zao zitabadilishwa kuwa kifungo cha maisha bila uwezekano wa kupewa msamaha.Wei, mwenye umri wa miaka 72, alihudumu kama waziri wa ulinzi kuanzia 2018 hadi 2023. Li, mwenye umri wa miaka 68, alichukua nafasi ya Wei na kushikilia wadhifa huo kwa chini ya miezi minane mwaka 2023.

    Wote wawili waliwekwa chini ya uchunguzi na kitengo cha kupambana na ufisadi cha jeshi mwaka 2023.

  • China yalaani vikali uvamizi wa Iran yasema ipo thabiti pamoja nayo

    China yalaani vikali uvamizi wa Iran yasema ipo thabiti pamoja nayo

    Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, ametangaza kuwa operesheni ya kijeshi inayoendelea dhidi ya Iran ni kinyume cha sheria, huku akisisitiza kuwa Beijing inaendelea kuiunga mkono Tehran katika kulinda uhuru na usalama wake wa kitaifa.

    Katika mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, Wang Yi alisifu msimamo wa wananchi wa Iran na jitihada za nchi hiyo katika kuendeleza diplomasia na kuzuia kuongezeka kwa mvutano katika eneo. Alibainisha kuwa China inapinga matumizi ya nguvu na kuendelea kwa vita ambavyo vina athari zinazowagusa sio tu Wairani bali pia mataifa ya dunia nzima.

    Kwa upande wake, Araghchi alieleza ukiukaji wa haki za kibinadamu na uvamizi wa kijeshi unaofanywa na Marekani na Israel dhidi ya Iran. Pia alishukuru msimamo wa China katika kulaani uvunjaji wa misingi ya sheria za Umoja wa Mataifa na matumizi mabaya ya Baraza la Usalama.Araghchi aliweka wazi kuwa Iran inaendelea na juhudi za kidiplomasia za kukomesha uvamizi dhidi yake.

    Aliongeza kuwa pamoja na uwezo wa kijeshi wa kujilinda, Iran pia inabaki thabiti katika kufuatilia suluhisho la kidiplomasia.