Blog

  • Msafara wa Sumud Flotilla: Wanaharakati 18wa Uturuki wakamatwa na Israel

    Msafara wa Sumud Flotilla: Wanaharakati 18wa Uturuki wakamatwa na Israel

    Jeshi la Israel limezuia msafara wa Global Sumud Flotilla katika maji ya kimataifa, na kukamata meli 21, kulingana na waandaaji wa msafara huo.Takribani wanaharakati 175, wakiwemo raia wa Uturuki, walikamatwa, huku meli 17 zikiwa zimefanikiwa kufika kwenye maji ya Ugiriki.

    Msafara huo, uliokuwa umebeba zaidi ya raia 400, ulikuwa na lengo la kupeleka misaada ya kibinadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza lililozingirwa.Uturuki imelaani operesheni hiyo ikiitaja kama “kitendo cha uharamia”, ikishutumu Israel kwa kukiuka sheria za kimataifa na kulenga msafara wa kibinadamu uliokuwa na lengo la kuangazia kuzorota kwa hali ya kibinadamu Gaza.

  • Trump asema Marekani inachunguza uwezekano wa kupunguza wanajeshi nchini Ujerumani

    Trump asema Marekani inachunguza uwezekano wa kupunguza wanajeshi nchini Ujerumani

    Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kupitia mtandao wake wa Truth Social kwamba Marekani kwa sasa inachunguza na kutathmini uwezekano wa kupunguza idadi ya wanajeshi wake walioko nchini Ujerumani.

    Ameongeza kuwa uchunguzi huo unaendelea na kwamba uamuzi wa mwisho kuhusu suala hilo unatarajiwa kutolewa katika muda mfupi.

    Awali ya wiki hii Donald Trump alionyesha kuchukizwa na kauli ya Kansela wa Ujerumani, Friedrich, aliyesema kwamba Marekani imedhalilishwa na Iran katika uvamizi wake wa nchi hiyo.

  • Mazungumzo ya Simu kati ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Kenyaa

    Mazungumzo ya Simu kati ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Kenyaa

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Seyed Abbas Araghchi, leo Jumatano amefanya mazungumzo ya simu na Musalia Mudavadi, Mkuu wa mawaziri na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu hali ya usalama katika eneo la Asia Magharibi na athari za vitendo vya uchokozi vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran kwa usalama wa kikanda.

    Pia waligusia madhara ya kiuchumi yanayotokana na hali hiyo kwa maeneo mengine duniani.Waziri Araghchi alieleza wasiwasi wake kuhusu hali ya ukosefu wa usalama katika eneo la Ghuba ya Uajemi na Mlango wa Hormuz, akisema kuwa imesababishwa na uchokozi wa kijeshi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.

    Alisisitiza umuhimu wa hatua madhubuti za kimataifa kwa ajili ya kulinda Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kuwawajibisha wahusika kwa ukiukaji wa sheria na uhalifu unaodaiwa kufanywa.

    AKwa upande wake, Waziri Mudavadi alisisitiza umuhimu wa kuheshimu uhuru wa kitaifa na uadilifu wa mipaka ya nchi, pamoja na kuepuka matumizi ya nguvu. Aidha, alieleza kuwa diplomasia ni nyenzo muhimu katika kuleta na kudumisha amani katika eneo hilo.

  • Afisa wa Iran Mohsen Rezaei aonya Marekani dhidi ya kuanzisha tena vita

    Afisa wa Iran Mohsen Rezaei aonya Marekani dhidi ya kuanzisha tena vita

    Afisa wa Iran, Mohsen Rezaei, alisema kuwa chaguo lenye madhara madogo zaidi kwa Marekani ni kukubali masharti kumi ya Iran.

    Alionya kwamba ikiwa Marekani itaanza tena vita, itakuwa janga kwa Washington, na akaongeza kuwa uvamizi wowote wa ardhini utasababisha idadi kubwa ya wanajeshi wa Marekani kukamatwa.

  • USS Gerald R. Ford itaondoka Mashariki ya Kati katika siku zijazo

    USS Gerald R. Ford itaondoka Mashariki ya Kati katika siku zijazo

    USS Gerald R. Ford itaondoka Mashariki ya Kati katika siku zijazo.

    Meli ya kubeba ndege USS Gerald R. Ford inatarajiwa kuondoka Mashariki ya Kati na kuanza kurejea Marekani katika siku zijazo, kulingana na The Wall Street Journal.

  • Ripoti: Sababu za Iran Kutoonyesha Dalili za Kurudi Nyuma

    Ripoti: Sababu za Iran Kutoonyesha Dalili za Kurudi Nyuma

    Jarida la Marekani la Foreign Policy limeangazia sababu zinazoeleza kwa nini Iran haijaonyesha dalili za kurudi nyuma licha ya shinikizo la kimataifa.

    Kwa mujibu wa uchambuzi huo, mkakati wa Rais wa Marekani, Donald Trump, ulikuwa kulenga sekta ya mafuta ya Iran kwa matumaini ya kulazimisha kusitishwa kwa uzalishaji katika maeneo muhimu ya mafuta. Hata hivyo, ripoti inaeleza kuwa Tehran imewahi kupitia mazingira kama hayo hapo awali na imefanikiwa kuyakabili.

    Katika kipindi cha miongo kadhaa ya vikwazo vya kiuchumi, Iran imejenga uzoefu mkubwa katika kukabiliana na shinikizo la kimataifa. Ripoti hiyo inaeleza kuwa, tofauti na matarajio ya Washington, hatua kama kufunga njia za usafirishaji au kuweka vikwazo rasmi haziwezi kusimamisha kikamilifu uzalishaji na biashara ya mafuta ya Iran.

    Aidha, Iran imeunda mitandao ya usambazaji wa nishati ambayo ni vigumu kufuatilia na kuizuia. Mitandao hiyo, kwa mujibu wa uchambuzi, inafanya kuwa changamoto kubwa kwa juhudi zozote za kuzuia mauzo ya mafuta ya nchi hiyo.

    Ripoti pia inaeleza kuwa wahandisi wa Iran wamebuni mbinu za hali ya juu za kulinda na kusimamia visima vya mafuta hata katika mazingira ya uzalishaji wa kiwango cha chini.Kwa upande mwingine, uchambuzi unaonyesha kuwa Iran imekuwa ikitumia nafasi yake katika Mlango wa Hormuz kama nyenzo ya kimkakati, hatua inayoweza kuongeza gharama za kisiasa na kiuchumi kwa upande wa Marekani.