Blog

  • Wanachama Watatu wa Civil Defense Wauawa Katika Shambulio la Israel Kusini mwa Lebanon

    Wanachama Watatu wa Civil Defense Wauawa Katika Shambulio la Israel Kusini mwa Lebanon

    Civil Defense ya Lebanon imetangaza kuuawa kwa wanachama wake watatu wakati wakifanya operesheni ya uokoaji baada ya shambulio la anga la Israel kugonga jengo katika eneo la Majdal Zoun, wilaya ya Tyre, kusini mwa Lebanon.Waliouawa wametajwa kuwa Hussein Al-Sati, Hadi Daher, na Hussein Ghadbouni.

  • Trump amvaa kansela wa Ujerumani baada ya kiongozi huyo kusema Marekani imedhalilishwa na Iran

    Trump amvaa kansela wa Ujerumani baada ya kiongozi huyo kusema Marekani imedhalilishwa na Iran

    Rais wa Marekani, Donald Trump, amemkosoa vikali Kansela wa Ujerumani Hasira ya Trump kwa Ujerumani kunatokana na kukiri kwake kudhalilishwa vibaya kwa Marekani mbele ya Iran.

    kufuatia kauli hiyo Rais wamarekani amedai kwamba Kansela wa Ujerumani haoni umiliki wa silaha za nyuklia kwa Iran kuwa ni tatizo kubwa.Trump amedai kuwa Kansela huyo wa Ujerumani “hajui anachokizungumza” na kwamba kauli kama hizo zinaweza kudhoofisha msimamo wa Marekani dhidi ya Iran.

    Aidha, Trump ameituhumu Ujerumani kwa, akisema si jambo la kushangaza kwamba nchi hiyo, kwa maoni yake, inafanya vibaya katika uchumi na maeneo mengine muhimu.

  • Israel Inafanya “Mauaji ya Mazingira” nchini Lebanon kwa Gharama ya Jumla ya Dola Bilioni 25

    Israel Inafanya “Mauaji ya Mazingira” nchini Lebanon kwa Gharama ya Jumla ya Dola Bilioni 25

    Wizara ya Mazingira ya Lebanon inasema kuwa Israel inafanya “mauaji ya mazingira” kusini mwa Lebanon, kulingana na ripoti mpya inayofafanua uharibifu mkubwa wa ikolojia wakati wa uvamizi wa 2023–2024.Ripoti hiyo ya kurasa 106, iliyotolewa na Baraza la Kitaifa la Utafiti wa Kisayansi la Lebanon, inaeleza kuwa operesheni za kijeshi za Israel “zilibadilisha kwa kiasi kikubwa mandhari ya kifizikia na ya ikolojia,” na kusababisha uharibifu wa muda mrefu kwa misitu, mashamba, mifumo ya maji, ubora wa hewa, na bioanuwai.Katika utangulizi wake, Waziri wa Mazingira Tamara El Zein alielezea uharibifu huo kuwa wa makusudi na wa kina, akionya kwamba madhara ya mazingira yanazidi ikolojia pekee na yanatishia afya ya umma, usalama wa chakula, riziki za watu, na uimara wa taifa.Ripoti hiyo inaorodhesha uharibifu mkubwa, ikiwemo hekta 5,000 za misitu zilizoangamizwa, hasara kubwa katika kilimo na miundombinu ya mifugo, pamoja na mamia ya mamilioni ya dola katika uharibifu na upotevu wa uzalishaji.#utaridi

  • Marabi (viongozi) wa Kiyahudi wa mrengo wa kisasa nchini Uingereza Waonya kuwa Mwelekeo wa Sasa wa Israel Unaweza Kudhoofisha Maadili na Utambulisho wa Kiyahudi

    Marabi (viongozi) wa Kiyahudi wa mrengo wa kisasa nchini Uingereza Waonya kuwa Mwelekeo wa Sasa wa Israel Unaweza Kudhoofisha Maadili na Utambulisho wa Kiyahudi

    Marabi wakuu wa Kiyahudi wa mrengo wa maendeleo nchini Uingereza wameonya kuwa mwelekeo wa sasa wa kisiasa wa Israel unawakilisha tishio kubwa kwa maadili na utambulisho wa Kiyahudi, wakisisitiza kuwa ukosoaji wa serikali ya Israel ni “wajibu wa Kiyahudi,” si kitendo cha kukosa uaminifu.Rabbi Charley Baginsky na Rabbi Josh Levy, wanaoongoza Uyahudi wa Maendeleo unaowakilisha takriban theluthi moja ya masinagogi nchini Uingereza, walisema kuwa mwelekeo wa Israel unaweza kuwa “hauendani na maadili ya Kiyahudi” na unaweza kuleta “tishio la kuwepo” kwa Uyahudi wenyewe.Levy alisema kuwa kujihusisha na sera za Israel ni sehemu ya “mazungumzo ya Kiyahudi ya milenia” kuhusu maadili na uwajibikaji, akidai kuwa Wayahudi hawawezi kutenganisha utambulisho wao wa kidini na matendo ya dola ya Israel.Baginsky aliongeza kuwa Uzayuni wa kidini lazima ujumuishe kutambua haki ya Wapalestina kujitawala, akipinga tafsiri za mrengo mkali wa kulia za Uzayuni zinazokuzwa na wanasiasa wa Israel.

  • Viongozi wa chama cha Trump “Republicans” wamtaka kumaliza vita vya Iran kabla ya uchaguzi

    Viongozi wa chama cha Trump “Republicans” wamtaka kumaliza vita vya Iran kabla ya uchaguzi

    Washington – Rais wa Marekani, Donald Trump, anafahamu kikamilifu athari za kisiasa ambazo vita vimeleta kwake na kwa chama chake, kwa mujibu wa vyanzo vitatu vinavyofahamu mashauriano ya hivi karibuni yaliyofanyika katika Ikulu ya Marekani.

    Vyanzo hivyo vimeiambia Reuters kuwa licha ya kuwepo kwa shinikizo kubwa la ndani linalotaka vita vikomeshwe, chaguo za kijeshi bado hazijaondolewa mezani. Hata hivyo, wanasema kuwa mipango mikubwa ya kijeshi, ikiwemo uwezekano wa uvamizi wa ardhini ndani ya Iran, imepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na wiki zilizopita.

    Kwa mujibu wa taarifa za Reuters, ripoti kutoka uwanjani zinaonyesha kuwa Iran imetumia kipindi cha usitishaji mapigano kuimarisha tena uwezo wake wa kiulinzi. Inadaiwa kuwa majeshi ya Iran yamekarabati na kurejesha vifaa vya kijeshi, ikiwa ni pamoja na ndege zisizo na rubani na ghala za makombora zilizoharibiwa katika mashambulizi ya awali.

    Hatua hizo zinaripotiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa gharama za kijeshi ambazo Marekani ingeweza kukabiliana nazo iwapo vita vingerejea.

  • “Mwisho wa mgawanyiko”: Bennett na Lapid waungana rasmi kumbwaga Netanyahu

    “Mwisho wa mgawanyiko”: Bennett na Lapid waungana rasmi kumbwaga Netanyahu

    Waziri wakuu wa zamani wa Israel, Naftali Bennett na Yair Lapid, wametangaza kuunganisha rasmi vyama vyao na kuunda tiketi ya pamoja ya kisiasa itakayojulikana kama “Pamoja – Ikiongozwa na Naftali Bennett.”

    Tangazo hilo lilitolewa Jumapili alasiri na msemaji wa Bennett. Akizungumza na waandishi wa habari katika mji wa pwani wa Herzliya saa chache baadaye, Bennett alisema uamuzi wa kuungana na Lapid ni “hatua ya kizalendo na ya Kizayuni zaidi” ambayo wamewahi kuchukua kwa ajili ya maslahi ya nchi yao. Alisisitiza pia kuwa hatua hiyo inaashiria mwisho wa mgawanyiko wa kisiasa.

    Bennett alieleza kuwa yeye na Lapid, ambaye kwa sasa ni kiongozi wa upinzani, wanaendelea mbele kwa lengo la kupata ushindi katika uchaguzi ujao. Aidha, alimkaribisha mwenyekiti wa chama cha Yashar, Gadi Eisenkot, kujiunga na muungano huo, akisema kuwa mlango bado uko wazi kwa vyama na viongozi wengine wanaotaka kushirikiana.