Lebo: Makkah

  • al Houthi: hatuwezi kufunzwa utukufu wa Makkah na aliyempa Epstein kitambaa cha al-Kaaba

    al Houthi: hatuwezi kufunzwa utukufu wa Makkah na aliyempa Epstein kitambaa cha al-Kaaba

    Katika hotuba yake ya kusisimua ya kuadhimisha Septemba 21, kiongozi wa Ansarallah, Abdul-Malik al-Houthi, ameibua mjadala mzito kuhusu uhalali wa utawala wa Saudi Arabia juu ya mji mtakatifu wa Makkah.

    Al-Houthi alisisitiza kuwa Makkah si milki ya Saudia, bali ni eneo takatifu kwa Waislamu wote duniani. Alikwenda mbali zaidi kwa kuhoji kihistoria kuwa Saudia haikurithi mji huo, bali iliuteka kwa nguvu mwaka 1924 kupitia mauaji ya kikatili ya wakazi wa Taif na kuondoa utawala wa kihashimi.

    Aidha, kiongozi huyo alisema kuwa utawala wa Saudia umejawa na rekodi ya uhalifu wa muda mrefu dhidi ya mahujaji wa Yemen. Lakini pia kiongozi huyo alisema Mwana mfalme wa Saudia aliyemtuza Jeffrey Epstein kipande cha Kiswa cha Al-Kaaba; kitendo alichokiita kuwa ni unajisi wa hali ya juu, katu hawezi kuufunza ulimwengu kuuheshimu mji wa Makkah.

  • Yemen Yakanusha Madai ya Mpango wa Kushambulia Makkah

    Yemen Yakanusha Madai ya Mpango wa Kushambulia Makkah

    Jeshi la Yemen linaloongozwa na Ansarullah limekanusha madai ya Saudi Arabia kwamba linapanga kufanya shambulio dhidi ya mji mtakatifu wa Makkah, likiyataja madai hayo kuwa sehemu ya kampeni ya propaganda dhidi ya Yemen.

    Katika taarifa yake, jeshi hilo limeeleza madai ya Saudi Arabia kuwa “uzushi na udanganyifu,” likisema yanalenga kupotosha maoni ya umma na kuchochea hisia dhidi ya Yemen katika eneo la Mashariki ya Kati.

    Uongozi wa Yemen umedai kuwa tuhuma hizo zinatumiwa na Riyadh kutafuta uungwaji mkono wa kisiasa na kidini wakati mvutano na mapigano katika eneo hilo yakiendelea.

    Yemen Yasisitiza Kuheshimu Maeneo Matakatifu

    Jeshi la Yemen linaloongozwa na Ansarullah limesisitiza kuwa linaheshimu maeneo matakatifu ya Kiislamu, likikanusha kuwa Makkah ni miongoni mwa maeneo yanayolengwa katika operesheni zake.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, operesheni zake za kijeshi zinalenga maeneo inayoyahusisha na shughuli za kijeshi za upande unaopambana nao.

    Kauli hiyo ni majibu ya moja kwa moja kwa madai yaliyohusishwa na Saudi Arabia kuhusu uwezekano wa shambulio dhidi ya Makkah.

    Vita vya Taarifa

    Madai kuhusu uwezekano wa kushambuliwa kwa Makkah yanaongeza mwelekeo mwingine katika vita vya taarifa vinavyoambatana na mvutano wa kijeshi katika eneo hilo.

    Saudi Arabia na Ansarullah zimekuwa zikitoa taarifa zinazokinzana kuhusu operesheni za kijeshi, malengo na matokeo yake. Katika mazingira hayo, madai kuhusu mpango wa kushambulia Makkah pamoja na maelezo ya kila upande kuhusu nia za mwenzake yanahitaji uthibitisho wa kujitegemea.

    Makkah ni mji mtakatifu zaidi katika Uislamu na eneo la Msikiti Mkuu unaozunguka Al-Kaaba, hivyo madai yoyote kuhusu tishio la kijeshi dhidi ya mji huo yana uzito mkubwa wa kidini, kisiasa na kiusalama katika ulimwengu wa Kiislamu.