Lebo: Marekani

  • USS Gerald R. Ford itaondoka Mashariki ya Kati katika siku zijazo

    USS Gerald R. Ford itaondoka Mashariki ya Kati katika siku zijazo

    USS Gerald R. Ford itaondoka Mashariki ya Kati katika siku zijazo.

    Meli ya kubeba ndege USS Gerald R. Ford inatarajiwa kuondoka Mashariki ya Kati na kuanza kurejea Marekani katika siku zijazo, kulingana na The Wall Street Journal.

  • Ripoti: Sababu za Iran Kutoonyesha Dalili za Kurudi Nyuma

    Ripoti: Sababu za Iran Kutoonyesha Dalili za Kurudi Nyuma

    Jarida la Marekani la Foreign Policy limeangazia sababu zinazoeleza kwa nini Iran haijaonyesha dalili za kurudi nyuma licha ya shinikizo la kimataifa.

    Kwa mujibu wa uchambuzi huo, mkakati wa Rais wa Marekani, Donald Trump, ulikuwa kulenga sekta ya mafuta ya Iran kwa matumaini ya kulazimisha kusitishwa kwa uzalishaji katika maeneo muhimu ya mafuta. Hata hivyo, ripoti inaeleza kuwa Tehran imewahi kupitia mazingira kama hayo hapo awali na imefanikiwa kuyakabili.

    Katika kipindi cha miongo kadhaa ya vikwazo vya kiuchumi, Iran imejenga uzoefu mkubwa katika kukabiliana na shinikizo la kimataifa. Ripoti hiyo inaeleza kuwa, tofauti na matarajio ya Washington, hatua kama kufunga njia za usafirishaji au kuweka vikwazo rasmi haziwezi kusimamisha kikamilifu uzalishaji na biashara ya mafuta ya Iran.

    Aidha, Iran imeunda mitandao ya usambazaji wa nishati ambayo ni vigumu kufuatilia na kuizuia. Mitandao hiyo, kwa mujibu wa uchambuzi, inafanya kuwa changamoto kubwa kwa juhudi zozote za kuzuia mauzo ya mafuta ya nchi hiyo.

    Ripoti pia inaeleza kuwa wahandisi wa Iran wamebuni mbinu za hali ya juu za kulinda na kusimamia visima vya mafuta hata katika mazingira ya uzalishaji wa kiwango cha chini.Kwa upande mwingine, uchambuzi unaonyesha kuwa Iran imekuwa ikitumia nafasi yake katika Mlango wa Hormuz kama nyenzo ya kimkakati, hatua inayoweza kuongeza gharama za kisiasa na kiuchumi kwa upande wa Marekani.

  • Trump ashindwa na mchezaji Snuka wa Iran

    Trump ashindwa na mchezaji Snuka wa Iran

    Hossein Vafaei wa Iran amepata ushindi muhimu baada ya kumshinda Judd Trump, anayeshika nafasi ya kwanza duniani katika mchezo wa snuka. Katika pambano lililodumu kwa raundi tatu, Vafaei alifanikiwa kumtungua Trump na kufuzu kuingia katika hatua ya wachezaji nane bora duniani. Ushindi huo unaimarisha nafasi ya Vafaei katika mashindano hayo na kuvutia macho ya wapenzi wa snuka duniani.Baada ya ushindi huo Hossein Vafaei ameingia miongoni mwa wachezaji 8 bora duniani.

  • Silaha za Nyuklia za Korea Kaskazini Zaibua Wasiwasi Mpya kwa Marekani

    Silaha za Nyuklia za Korea Kaskazini Zaibua Wasiwasi Mpya kwa Marekani

    Korea Kaskazini inakaribia kufikia kiwango ambapo uwezo wake wa silaha za nyuklia unaweza kuzidi mifumo ya ulinzi wa makombora ya Marekani, kulingana na taarifa za hivi karibuni.

    Marekani kwa sasa ina vizuia‑makombora 44 vya ardhini vinavyokusudiwa kukabiliana na makombora ya masafa marefu, idadi ambayo inakadiriwa kuwa na uwezo wa kuzuia takriban makombora 20 hadi 25 yanayoingia.

    Wakati huohuo, Korea Kaskazini inaendelea kuongeza kasi ya uzalishaji wa silaha zake za nyuklia, ikitengeneza takriban vichwa vya nyuklia 12 hadi 15 kila mwaka. Aidha, nchi hiyo inaendelea kupanua ghala lake la makombora ya masafa marefu ya bara hadi bara (ICBM), ikiwa ni pamoja na kuanzisha makombora mapya na mifumo ya chambo (decoy) inayolenga kufanya juhudi za kuyazuia kuwa ngumu zaidi, kwa mujibu wa Bloomberg.

  • Trump amvaa kansela wa Ujerumani baada ya kiongozi huyo kusema Marekani imedhalilishwa na Iran

    Trump amvaa kansela wa Ujerumani baada ya kiongozi huyo kusema Marekani imedhalilishwa na Iran

    Rais wa Marekani, Donald Trump, amemkosoa vikali Kansela wa Ujerumani Hasira ya Trump kwa Ujerumani kunatokana na kukiri kwake kudhalilishwa vibaya kwa Marekani mbele ya Iran.

    kufuatia kauli hiyo Rais wamarekani amedai kwamba Kansela wa Ujerumani haoni umiliki wa silaha za nyuklia kwa Iran kuwa ni tatizo kubwa.Trump amedai kuwa Kansela huyo wa Ujerumani “hajui anachokizungumza” na kwamba kauli kama hizo zinaweza kudhoofisha msimamo wa Marekani dhidi ya Iran.

    Aidha, Trump ameituhumu Ujerumani kwa, akisema si jambo la kushangaza kwamba nchi hiyo, kwa maoni yake, inafanya vibaya katika uchumi na maeneo mengine muhimu.

  • Viongozi wa chama cha Trump “Republicans” wamtaka kumaliza vita vya Iran kabla ya uchaguzi

    Viongozi wa chama cha Trump “Republicans” wamtaka kumaliza vita vya Iran kabla ya uchaguzi

    Washington – Rais wa Marekani, Donald Trump, anafahamu kikamilifu athari za kisiasa ambazo vita vimeleta kwake na kwa chama chake, kwa mujibu wa vyanzo vitatu vinavyofahamu mashauriano ya hivi karibuni yaliyofanyika katika Ikulu ya Marekani.

    Vyanzo hivyo vimeiambia Reuters kuwa licha ya kuwepo kwa shinikizo kubwa la ndani linalotaka vita vikomeshwe, chaguo za kijeshi bado hazijaondolewa mezani. Hata hivyo, wanasema kuwa mipango mikubwa ya kijeshi, ikiwemo uwezekano wa uvamizi wa ardhini ndani ya Iran, imepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na wiki zilizopita.

    Kwa mujibu wa taarifa za Reuters, ripoti kutoka uwanjani zinaonyesha kuwa Iran imetumia kipindi cha usitishaji mapigano kuimarisha tena uwezo wake wa kiulinzi. Inadaiwa kuwa majeshi ya Iran yamekarabati na kurejesha vifaa vya kijeshi, ikiwa ni pamoja na ndege zisizo na rubani na ghala za makombora zilizoharibiwa katika mashambulizi ya awali.

    Hatua hizo zinaripotiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa gharama za kijeshi ambazo Marekani ingeweza kukabiliana nazo iwapo vita vingerejea.