Lebo: Michezo

  • MWISHO WA ENZI: Pep Guardiola Kuiaga Manchester City, Enzo Maresca Atajwa Kurithi Mikoba Yake

    MWISHO WA ENZI: Pep Guardiola Kuiaga Manchester City, Enzo Maresca Atajwa Kurithi Mikoba Yake

    Kocha mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola, anatarajiwa kuachia ngazi majira ya joto mwaka huu, hatua itakayohitimisha moja ya vipindi vya mafanikio makubwa zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya England (Premier League).

    Vyanzo mbalimbali vya habari vilivyo karibu na klabu hiyo vinaeleza kuwa, Guardiola anajiandaa kuondoka mwishoni mwa msimu huu ambao tayari kikosi chake kimeshatwaa makombe ya Carabao na FA.

    Ushindi wa Jumamosi dhidi ya Chelsea umemhakikishia kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 taji lake la 20 kubwa ndani ya kipindi cha miaka 10 aliyodumu kunako dimba la Etihad.

    Kufuatia taarifa hizo, aliyekuwa kocha wa Chelsea, Enzo Maresca, anapewa nafasi kubwa ya kwenda kuchukua mikoba ya kuinoa miamba hiyo ya soka. Maresca anatarajiwa kupewa jukumu hilo zikiwa zimepita miezi minne pekee tangu aondoke Chelsea, huku Manchester City ikisalia kwenye nafasi nzuri ya kuweza kutwaa ubingwa mwingine wa Ligi Kuu msimu huu.

  • Crystal Palace yatinga fainali ya Conference League Ulaya baada ya kuifunga tena Shakhtar Donetsk

    Crystal Palace yatinga fainali ya Conference League Ulaya baada ya kuifunga tena Shakhtar Donetsk

    Crystal Palace imefanikiwa kutinga fainali ya Ligi ya Mkutano Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali uliochezwa Alhamisi.

    Timu hiyo ya England ilionyesha ubora wake tena baada ya pia kushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-1, hivyo kufuzu kwa jumla ya mabao 5-2 katika michezo yote miwili.

    Katika mchezo huo, bao la kwanza la Crystal Palace lilipatikana dakika ya 25 kufuatia Pedro Henrique wa Shakhtar kujifunga.

    Ismaïla Sarr aliiongezea Palace bao la pili dakika ya 52 na kuimarisha matumaini ya timu hiyo kufuzu.Shakhtar Donetsk walipata bao lao pekee dakika ya 34 kupitia kwa Eguinaldo, lakini halikutosha kuizuia Crystal Palace kusonga mbele hadi hatua ya fainali.

    Kwa ushindi huo, Crystal Palace sasa itakutana na Rayo Vallecano ya Hispania katika fainali ya michuano hiyo, itakayochezwa tarehe 27 Mei mjini Leipzig, Ujerumani.

  • Trump ashindwa na mchezaji Snuka wa Iran

    Trump ashindwa na mchezaji Snuka wa Iran

    Hossein Vafaei wa Iran amepata ushindi muhimu baada ya kumshinda Judd Trump, anayeshika nafasi ya kwanza duniani katika mchezo wa snuka. Katika pambano lililodumu kwa raundi tatu, Vafaei alifanikiwa kumtungua Trump na kufuzu kuingia katika hatua ya wachezaji nane bora duniani. Ushindi huo unaimarisha nafasi ya Vafaei katika mashindano hayo na kuvutia macho ya wapenzi wa snuka duniani.Baada ya ushindi huo Hossein Vafaei ameingia miongoni mwa wachezaji 8 bora duniani.