Lebo: Oman

  • Mufti wa Oman awataka Waislamu kuunga mkono Iran na Gaza

    Mufti wa Oman awataka Waislamu kuunga mkono Iran na Gaza

    Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmed Al‑Khalili, ametoa wito kwa Waislamu duniani kuonyesha mshikamano wao na Iran na Gaza kufuatia maendeleo ya hivi karibuni katika eneo la Mashariki ya Kati.

    Katika kauli yake kuhusu hali ya eneo hilo, Sheikh Al‑Khalili alisisitiza umuhimu wa umoja wa ulimwengu wa Kiislamu mbele ya mashambulizi yanayolenga nchi na maeneo ya Kiislamu.

    Amesema Waislamu wanapaswa kusimama pamoja na kuonyesha mshikamano dhidi ya aina yoyote ya uchokozi unaolenga Gaza, Iran au sehemu nyingine za ardhi za Kiislamu.

    Mufti huyo pia alisisitiza kuwa Umma wa Kiislamu ni umma mmoja, na kwamba umoja na mshikamano ni muhimu katika kukabiliana na changamoto na mashambulizi dhidi ya nchi za Kiislamu.

  • Oman na Iran zafanya mazungumzo juu ya usalama wa Hormuz

    Oman na Iran zafanya mazungumzo juu ya usalama wa Hormuz

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amesema kuwa mazungumzo aliyofanya na mwenzake wa Iran kuhusu Mlango wa Hormuz yalikuwa na tija.Ameeleza kuwa kuna umuhimu wa kuimarisha juhudi za kidiplomasia pamoja na kutafuta suluhisho za vitendo ili kuhakikisha uhuru wa urambazaji – mchakato wa kuelekeza na kusimamia mwendo wa chombo cha usafiri kama meli, ndege, au hata gari kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa usalama na ufanisi – katika eneo hilo unadumishwa kwa muda mrefu.