Mwandishi: Suleiman Ali

  • Medvedev: Malumbano ya Marekani na Ulaya ni ushindi mkubwa kwa Urusi

    Medvedev: Malumbano ya Marekani na Ulaya ni ushindi mkubwa kwa Urusi

    Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi, Dmitry Medvedev, amesema kuwa mvutano unaoendelea kati ya Marekani na nchi za Ulaya unaweza hatimaye kupelekea ushindi kwa Urusi.

    Akizungumza kuhusu hali ya kisiasa ya kimataifa, Medvedev alieleza kuwa ni “jambo la kufurahisha” kutazama jinsi mahusiano kati ya Marekani na Ulaya yanavyozorota siku hadi siku.Wachambuzi wa kisiasa wanaona kauli hiyo kama ishara ya kujiamini kwa Urusi katika mazingira ambamo uhusiano wa Marekani na mataifa mengine duniani unaonekana kuzorota.

  • Mpango wa Trump kuhusu Gaza waanza kufeli; kituo cha CMCC kufungwa

    Mpango wa Trump kuhusu Gaza waanza kufeli; kituo cha CMCC kufungwa

    WASHINGTON – Mpango wa amani wa Rais Trump nchini Gaza unaonekana kulegalega kufuatia uamuzi wa Marekani wa kufunga kituo chake kikuu cha uratibu wa kijeshi (CMCC).

    Hatua hii inajiri huku kukiwa na ukosoaji mkubwa kwamba kituo hicho kimeshindwa kusimamia makubaliano ya kusitisha mapigano au kuboresha hali ya utoaji wa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo.Inaripotiwa kuwa shughuli za kituo hicho sasa zitahamishiwa chini ya usimamizi wa kikosi kipya cha kimataifa, ambacho kitakuwa na idadi ndogo ya wanajeshi wa Marekani ikilinganishwa na hapo awali.

    Hata hivyo, wachambuzi wa mambo wanasema kuwa mustakabali wa mpango huo mzima bado ni wa mashaka. Hii inatokana na kuendelea kwa mashambulizi kutoka kwa jeshi la Israel huku kundi la Hamas likionekana bado limeimarika katika ngome zake, jambo linalofanya juhudi za kuleta utulivu kukwama na kukubaki kwenye hali ya sintofahamu.

    Chanzo: Reuters

  • Trump aendeleza Mashambulizi yake dhidi ya kiongozi wa Ujerumani

    Trump aendeleza Mashambulizi yake dhidi ya kiongozi wa Ujerumani

    Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kumkosoa vikali Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, katika chapisho lake la Truth social akisema kwamba anapaswa kuelekeza juhudi zaidi katika jitihada za kukomesha vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine, ambavyo amedai kwamba hadi sasa havijaonyesha mafanikio makubwa chini ya uongozi wake.

    Ameongeza kuwa kiongozi huyo pia anapaswa kushughulikia changamoto zinazokabili taifa lake, ikiwemo masuala ya uhamiaji na nishati, badala ya kujihusisha na mambo yanayohusu mataifa yanayopambana kutokomeza tishio la nyuklia la Iran.Kwa mujibu wa Rais wa Marekani, Donald J. Trump, hatua hizo zingesaidia kuifanya dunia, ikiwemo Ujerumani, kuwa mahali salama zaidi.

  • Chombo cha habari cha Kizayuni channel 12: Netanyahu amekuwa alama ya “Shetani”

    Chombo cha habari cha Kizayuni channel 12: Netanyahu amekuwa alama ya “Shetani”

    Chombo cha habari cha kiisraeli “Channel 12” katika uchambuzi wake kimeashiria kuporomoka pakubwa kwa nafasi ya Israel katika kiwango cha kimataifa.

    Katika uchambuzi huo, mtandao huo umekiri kuwa jina la Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwa watu wengi duniani limeanza kuonekana kama alama ya “shetani”, jambo linaloonyesha kuongezeka kwa ukosoaji na mtazamo hasi dhidi ya Israel na uongozi wake katika jamii ya kimataifa.

  • Msafara wa Sumud Flotilla: Wanaharakati 18wa Uturuki wakamatwa na Israel

    Msafara wa Sumud Flotilla: Wanaharakati 18wa Uturuki wakamatwa na Israel

    Jeshi la Israel limezuia msafara wa Global Sumud Flotilla katika maji ya kimataifa, na kukamata meli 21, kulingana na waandaaji wa msafara huo.Takribani wanaharakati 175, wakiwemo raia wa Uturuki, walikamatwa, huku meli 17 zikiwa zimefanikiwa kufika kwenye maji ya Ugiriki.

    Msafara huo, uliokuwa umebeba zaidi ya raia 400, ulikuwa na lengo la kupeleka misaada ya kibinadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza lililozingirwa.Uturuki imelaani operesheni hiyo ikiitaja kama “kitendo cha uharamia”, ikishutumu Israel kwa kukiuka sheria za kimataifa na kulenga msafara wa kibinadamu uliokuwa na lengo la kuangazia kuzorota kwa hali ya kibinadamu Gaza.

  • Trump asema Marekani inachunguza uwezekano wa kupunguza wanajeshi nchini Ujerumani

    Trump asema Marekani inachunguza uwezekano wa kupunguza wanajeshi nchini Ujerumani

    Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kupitia mtandao wake wa Truth Social kwamba Marekani kwa sasa inachunguza na kutathmini uwezekano wa kupunguza idadi ya wanajeshi wake walioko nchini Ujerumani.

    Ameongeza kuwa uchunguzi huo unaendelea na kwamba uamuzi wa mwisho kuhusu suala hilo unatarajiwa kutolewa katika muda mfupi.

    Awali ya wiki hii Donald Trump alionyesha kuchukizwa na kauli ya Kansela wa Ujerumani, Friedrich, aliyesema kwamba Marekani imedhalilishwa na Iran katika uvamizi wake wa nchi hiyo.