Kategoria: MASHARIKI YA KATI

  • New York Times: Meli zimekataa kuvuka Mlango wa Hormuz licha ya kauli ya Trump

    New York Times: Meli zimekataa kuvuka Mlango wa Hormuz licha ya kauli ya Trump

    Makampuni ya usafirishaji baharini yameripotiwa kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kutuma meli zao kupita katika Mlango wa Hormuz, mojawapo ya njia muhimu zaidi za usafirishaji wa mafuta duniani. Baadhi ya kampuni hizo zinasema kuwa pendekezo la Marekani halijatosha kuwapa uhakika wa usalama unaohitajika.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wawakilishi wa sekta ya usafirishaji wameeleza kuwa hali ya usalama katika eneo hilo bado ni tete, jambo linalosababisha tahadhari kubwa kabla ya kufanya maamuzi ya kupeleka meli katika mkondo huo.Makampuni hayo pia yamesisitiza kuwa ili idadi kubwa ya vyombo vya baharini ivuke kwa usalama katika Mlango wa Hormuz, ni muhimu kwa Iran kushirikishwa katika mpango au makubaliano yoyote yatakayofikiwa. Wanasema ushirikiano wa pande zote ni muhimu kwa kuhakikisha uthabiti na usalama wa njia hiyo ya kimkakati.

  • Kimya cha kushangaza cha al‑Joulani juu ununuzi wa ardhi za Syria na mashirika ya kiyahudi

    Kimya cha kushangaza cha al‑Joulani juu ununuzi wa ardhi za Syria na mashirika ya kiyahudi

    Vyombo vya habari vya Kiarabu vimeripoti kuongezeka kwa ununuzi wa ardhi za kilimo kusini mwa Syria unaofanywa na watu wenye uraia wa nchi mbili wanaodaiwa kuwa na uhusiano na mashirika ya Kiyahudi.

    Ripoti hizo pia zinataja kuwepo kwa harakati nyingine sambamba, zikiwemo ziara za ujumbe wa Israeli katika maeneo mbalimbali ya Syria pamoja na ununuzi wa baadhi ya maeneo ya zamani ya kijeshi ya Syria. Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mfululizo wa matukio haya unaonekana kuwa na uratibu maalum badala ya kuwa matukio ya bahati nasibu.

    Wachambuzi wanasema hatua hizi zinaonekana kuendana na kauli za baadhi ya viongozi wa harakati za ujenzi wa makazi ya walowezi wa Israeli, akiwemo Waziri wa Fedha wa Israel, Bezalel Smotrich, ambaye mara kadhaa amezungumzia wazo la mradi unaojulikana kama “Israel Kubwa”.

    Wakati maendeleo haya yakiripotiwa kusini mwa Syria, serikali ya waasi inayoongozwa na al‑Joulani imetajwa na baadhi ya wachambuzi kuwa haijatoa msimamo wa wazi kuhusu suala hilo, huku pia kukiwa na taarifa za kuwepo kwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya upande huo na Israel.

  • Iran yaishutumu UAE kwa ushirikiano na Marekani na Israel, yaonya kuhusu hatua ya kujibu

    Iran yaishutumu UAE kwa ushirikiano na Marekani na Israel, yaonya kuhusu hatua ya kujibu

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeilaani Abu Dhabi kwa kushirikiana na Marekani na Israel dhidi ya Iran, hasa kwa kuruhusu kuwepo kwa kambi za kijeshi na vifaa vya kijeshi.

    Tehran pia imekataa madai kwamba ilirusha makombora au ndege zisizo na rubani kuelekea UAE, ikisema kuwa hatua zake zinalenga tu kukabiliana na uchokozi wa Marekani.

    Wizara hiyo imeonya kuwa kuendelea kwa ushirikiano wa kijeshi au wa vifaa dhidi ya Iran hakukubaliki, na kusisitiza kwamba Iran itachukua hatua zote zinazohitajika kulinda usalama wake wa kitaifa.

  • Iran yakana tuhuma za mashambulizi UAE yasema sio kawaida yake kuficha mapigo

    Iran yakana tuhuma za mashambulizi UAE yasema sio kawaida yake kuficha mapigo

    Msemaji wa Makao Makuu ya Khatam al‑Anbiya amesema kuwa Iran itatoa “jibu kali na la kuangamiza” iwapo hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya nchi hiyo itafanywa kutoka ardhi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).a

    Katika taarifa yake, msemaji huyo alikanusha ripoti iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya UAE akidai kuwa katika siku za hivi karibuni vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran havijafanya operesheni yoyote ya makombora au ndege zisizo na rubani dhidi ya UAE.

    Alisisitiza kuwa iwapo operesheni kama hiyo ingefanyika, Iran ingeitangaza wazi na bila kusita.Taarifa hiyo pia iliwaonya viongozi wa UAE kwamba nchi yao, kama ardhi ya Kiislamu, haipaswi kuwa kituo au makazi ya vikosi na vifaa vya kijeshi vya Marekani na Israel. Kwa mujibu wa msemaji huyo, hatua kama hizo zinachukuliwa kuwa usaliti dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu.

    Aidha, msemaji huyo aliitaka UAE kuepuka kile alichokiita “mtego wa Marekani na Wazayuni,” akisema badala ya kuishambulia Iran kupitia propaganda za vyombo vya habari na tuhuma zisizo na msingi, nchi hiyo inapaswa kujiepusha na ushirikiano na mataifa yanayochukuliwa kuwa maadui wa ulimwengu wa Kiislamu.Katika taarifa hiyo, ilielezwa pia kuwa kwa sasa UAE imekuwa moja ya vituo muhimu vya uwepo wa kijeshi wa Marekani na Israel katika eneo la Mashariki ya Kati, jambo ambalo Iran inaliona kuwa chanzo kikuu cha ukosefu wa usalama katika kanda hiyo.

    Msemaji huyo aliongeza kuwa Iran imekuwa ikionyesha uvumilivu dhidi ya kile alichokiita propaganda na msaada wa UAE kwa maadui wa Iran na wa ulimwengu wa Kiislamu, akisema hatua hiyo imechukuliwa kwa kuzingatia usalama wa Waislamu wanaoishi katika nchi hiyo.

    Hata hivyo, alionya kwamba ikiwa ardhi ya UAE itatumika kufanya mashambulizi dhidi ya visiwa vya Iran, bandari au fukwe zake, Iran itajibu kwa nguvu na hatua ambayo itasababisha majuto

  • Waziri Araqchi: suluhu ya kijeshi ni jambo lisilowezekana

    Waziri Araqchi: suluhu ya kijeshi ni jambo lisilowezekana

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Seyed Abbas Araghchi, amesema kuwa matukio ya karibuni katika Mlango wa Bahari wa Hormuz yameweka wazi tena kwamba hakuna suluhisho la kijeshi kwa mgogoro wa kisiasa unaoikumba kanda ya Asia Magharibi, akisisitiza upya sera ya Jamhuri ya Kiislamu ya kufuatilia diplomasia kutoka katika nafasi ya nguvu.

    Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X usiku wa Jumatatu, Araghchi ameeleza kuwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani yanaendelea kupiga hatua kwa uthabiti, huku akizipongeza juhudi za Pakistan kwa upatanishi wake wa dhati na wenye kujenga.

    Amesema: “Mazungumzo yanapoendelea kupata mafanikio kutokana na juhudi za Pakistan, Marekani inapaswa kuwa makini isije ikavutwa tena katika dimbwi la matatizo na wale wasiolitakia mema eneo hili. Vivyo hivyo kwa Umoja wa Falme za Kiarabu.”

    Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Iran pia amekosoa vikali kile ambacho Washington imekuwa ikikitangaza sana kama “Mradi wa Uhuru” wenye lengo la kuongeza mashinikizo ya kijeshi katika Mlango wa Hormuz na ameutaja mpango huo kuwa “ Mradi wa Mkwamo.”

    Kauli za Araghchi zinakuja wakati ambapo Jamhuri ya Kiislamu, kupitia uwezo wake wa kujihami na udhibiti wake thabiti katika njia hiyo ya kimkakati ya baharini, imeweza kuthibitisha kwamba jaribio lolote la kutaka kulazimisha matokeo kwa nguvu au vitisho halitaweza kufanikiwa.

  • Makombora Mawili Yapiga Meli ya Kivita ya Marekani Baada ya Kupuuza Onyo la Iran

    Makombora Mawili Yapiga Meli ya Kivita ya Marekani Baada ya Kupuuza Onyo la Iran

    JASK, IRAN — Vyanzo vya habari vya eneo la Kusini vimeripoti tukio la mashambulizi ya makombora mawili yaliyolenga meli ya kivita ya Marekani katika maji ya karibu na Jask, nchini Iran. Tukio hilo limetokea leo Jumatatu, baada ya meli hiyo kudaiwa kuvunja kanuni za usalama wa usafiri na kujaribu kupita katika Bahari nyembamba ya Hormuz bila kibali rasmi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

    Kwa mujibu wa ripoti hizo, meli ya Marekani ilipuuzia onyo lililotolewa na Jeshi la Wanamaji la Iran, hali iliyosababisha kushambuliwa kwa makombora. Baada ya mashambulizi hayo, meli hiyo ilishindwa kuendelea na safari yake na kulazimika kuondoka kwa haraka kutoka eneo la tukio.

    Serikali ya Iran imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kwamba meli zote za kivita na za kibiashara lazima zipate kibali rasmi kabla ya kupita katika Bahari ya Hormuz. Imeonya kwamba kupuuza agizo hilo kutajibiwa kwa hatua kali na jeshi.

    Mpaka kufikia wakati wa kuandaa taarifa hii, hakuna maelezo ya kina yaliyotolewa kuhusu kiwango cha uharibifu au idadi ya vifo na majeruhi.

    Chanzo: Vyanzo vya habari vya ndani