Lebo: habari

  • Trump Aitaka Iran Kutoa Jibu la Haraka kwa Pendekezo lake la Amania

    Trump Aitaka Iran Kutoa Jibu la Haraka kwa Pendekezo lake la Amania

    Kituo cha Al-Arabiya kikinukuu chanzo cha serikali ya Pakistan kimeripoti kuwa Rais wa Marekani ameiomba Iran kutoa jibu la haraka kwa pendekezo la amani lililotumwa na Washington. Kwa mujibu wa chanzo hicho, Iran huenda ikawasilisha jibu hilo leo kupitia Serikali ya Pakistan.

    Chanzo hicho kimeeleza kuwa mawasiliano kati ya maafisa wa Pakistan na Iran bado yanaendelea bila changamoto yoyote, na kwamba hakuna kikwazo kinachozuia pande hizo mbili kuendeleza mazungumzo au kubadilishana taarifa.

    Aidha, katika mazungumzo hayo, chanzo cha Pakistani kimetaja umuhimu wa Mlango Bahari wa Hormuz na kusema kuwa suluhisho la muda mrefu kuhusu eneo hilo nyeti la kimkakati linaonekana kuwa ndani ya uwezo wa kufikiwa.

  • Rais Tshisekedi aazimia kugombea muhula wa tatu wa urais, Kongo

    Rais Tshisekedi aazimia kugombea muhula wa tatu wa urais, Kongo

    Rais Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amezungumzia uwezekano wa kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tatu, akisema atakubali kuendelea kuiongoza nchi hiyo iwapo ataungwa mkono na Wakongo kupitia kura ya maoni.Akizungumza katika mkutano na wanahabari siku ya Jumatano, Tshisekedi mwenye umri wa miaka 62 alisisitiza kuwa binafsi hakutaka kuongeza muda wake wa kukaa madarakani zaidi ya kikomo cha mihula miwili kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Kidmeokrasia ya Kongo unaomalizika mwaka wa 2028.“Sijawahi kufikia kuwania muhula wa tatu, lakini ninawaambia: Kama wananchi wa Kongo wanataka niendelee na muhula wa tatu, nitakubali,” amesema Rais wa Felix Tshisekedi.Ameongeza kuwa: Marekebisho yoyote ya Katiba yanayoruhusu hatua hiyo yatafanyika tu kwa idhini ya umma.Tshisekedi pia ametahdharisha kuwa mzozo unaoendelea mashariki mwa Kongo unaweza kupelekea kuahirishwa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika 2028.Mapigano kati ya wanajeshi wa Kongo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda yameongezeka katika majimbo yenye utajiri wa madini ya Kivu Kaskazini na Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

  • Wakristo nchini Lebanon walaani vikali jeshi vamizi la Israel kukosea heshima matukufu yao

    Wakristo nchini Lebanon walaani vikali jeshi vamizi la Israel kukosea heshima matukufu yao

    Wakatoliki nchini Lebanon wameeleza masikitiko yao kufuatia picha iliyoenea mtandaoni ikimuonyesha askari wa Israeli akivuta sigara akiwa ameishirikisha sanamu ya Bikira Maria.

    Tukio hilo liliripotiwa kutokea katika kijiji cha Kikristo cha Debel, kusini mwa Lebanon.Kwa mujibu wa vyanzo vya eneo hilo, kijiji cha Debel ndicho hicho hicho ambako mwezi uliopita askari wa Israeli alihusishwa na kitendo cha kuvunja sanamu ya Yesu Kristo.

    Matukio hayo yamezua hofu na malalamiko miongoni mwa jumuiya za Kikristo nchini Lebanon, ambazo zinadai visa vya askari wa Israeli kudhihirisha kutoheshimu imani yao vinaendelea kuongezeka.

  • Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kwamba “Project Freedom,” mpango unaoongozwa na Marekani kwa ajili ya harakati za meli kupitia Mlango wa Hormuz, utasitishwa kwa muda.

    Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kwamba “Project Freedom,” mpango unaoongozwa na Marekani kwa ajili ya harakati za meli kupitia Mlango wa Hormuz, utasitishwa kwa muda.

    Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kusitishwa kwa muda kwa mpango unaojulikana kama “Project Freedom,” ambao ni mpango unaoongozwa na Marekani uliolenga kuratibu na kulinda harakati za meli zinazopita katika Mlango wa Hormuz.

    Taarifa hiyo ilitolewa katika taarifa rasmi, ambapo Trump alieleza kuwa kusitishwa huko ni kwa muda huku tathmini zaidi kuhusu hatua zinazofuata ikiendelea kufanywa.

    Je, ni kweli Trump anafanya tathmini au Project imefeli ya kumtoa Muajemi?

  • Serikali ya Kenya Yashukuru Mapokezi ya Tanzania, Yaahidi Kuimarisha Ushirikiano wa Kikanda

    Serikali ya Kenya Yashukuru Mapokezi ya Tanzania, Yaahidi Kuimarisha Ushirikiano wa Kikanda

    Serikali ya Kenya imetoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, pamoja na wananchi wa Tanzania kwa mapokezi ya kipekee na ukarimu waliouonyesha wakati wa Ziara ya Kihistoria ya Kitaifa iliyofanyika nchini humo.

    Kupitia taarifa rasmi, Serikali ya Kenya imesisitiza dhamira yake ya kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yaliyosainiwa wakati wa ziara hiyo, ambayo yanalenga kuimarisha maendeleo ya pamoja na kukuza ustawi wa mataifa hayo mawili.

    Serikali hiyo pia imeeleza kuwa itaendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa pande mbili kati ya Kenya na Tanzania, sambamba na kuendeleza ushirikiano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa lengo la kuongeza muunganiko wa kikanda na ustawi wa pamoja.

    Ziara hiyo ya Kitaifa ya siku mbili ilihitimishwa kwa hafla ya kuagana rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Dodoma, baada ya majadiliano yenye mafanikio kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.

  • Trump Abadilisha Tena Ratiba ya Kumalizika kwa Uvamizi Dhidi ya Iran

    Trump Abadilisha Tena Ratiba ya Kumalizika kwa Uvamizi Dhidi ya Iran

    Washington, DC — Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza tena muda mpya wa kumalizika kwa vita dhidi ya Iran, akisema kuwa mapigano hayo huenda yakachukua “wiki mbili hadi tatu zaidi”.

    Hii si mara ya kwanza kwa rais huyo kubadilisha makadirio yake kuhusu muda wa vita. Mwanzoni mwa mapigano, Trump alikuwa ametaja kuwa vita vinaweza kudumu “wiki nne au tano”.

    Hata hivyo, wiki mbili baadaye, katika mkutano na waandishi wa habari, alisema: “Tutajiondoa hivi karibuni sana. Labda ndani ya wiki mbili, wiki mbili, labda wiki tatu.”Aidha, tarehe 12 Farvardin, katika hotuba yake katika Ikulu ya White House, Trump alitabiri kuwa vita vitaisha “ndani ya siku tatu zijazo”.

    Wachambuzi wa masuala ya kimataifa wameeleza kuwa kauli zinazotofautiana za rais huyo zimeibua maswali kuhusu mkakati wa Marekani.

    Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa moja ya sababu za ujumbe unaokinzana wa Trump kuhusu Iran ni kwamba “makadirio yake kuhusu Iran yaligeuka kuwa ya makosa.”Maendeleo zaidi yanatarajiwa huku hali ikiendelea kufuatiliwa kwa karibu.w