Lebo: utaridi

  • China yawahukumu kifo mawaziri wawili wa zamani wa ulinzi

    China yawahukumu kifo mawaziri wawili wa zamani wa ulinzi

    Beijing — Katika hatua ya kushangaza huku kukiendelea msako ndani ya jeshi lake, China siku ya Alhamisi iliwapa mawaziri wake wawili wa zamani wa ulinzi adhabu ya kifo iliyoahirishwa kwa tuhuma za ufisadi.

    Wei Fenghe na Li Shangfu wote walipatikana na hatia ya kupokea rushwa na wakahukumiwa adhabu ya kifo yenye kusitishwa kwa miaka miwili na mahakama ya kijeshi ya nchi hiyo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.

    Mahakama ilitangaza kuwa baada ya miaka miwili, adhabu zao zitabadilishwa kuwa kifungo cha maisha bila uwezekano wa kupewa msamaha.Wei, mwenye umri wa miaka 72, alihudumu kama waziri wa ulinzi kuanzia 2018 hadi 2023. Li, mwenye umri wa miaka 68, alichukua nafasi ya Wei na kushikilia wadhifa huo kwa chini ya miezi minane mwaka 2023.

    Wote wawili waliwekwa chini ya uchunguzi na kitengo cha kupambana na ufisadi cha jeshi mwaka 2023.

  • Ufaransa: “Tunalipa gharama ya vita ambavyo hatukuvichagua”

    Ufaransa: “Tunalipa gharama ya vita ambavyo hatukuvichagua”

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa ameonya kuwa uwezekano wa kuondoa vikwazo dhidi ya Iran haupo kabisa hadi pale Mlango wa Hormuz utakapofunguliwa, akibainisha msimamo mkali wa Paris kuhusu hali inayoendelea katika eneo la Asia ya Magharibi.
    Akizungumza leo kwenye mahojiano maalum na kituo cha redio na televisheni cha RTL, waziri huyo aliweka wazi misimamo miwili mikuu: Kwanza, kusisitiza kuwa hatua yoyote ya kuondoa vikwazo haitazingatiwa wakati njia muhimu ya kimkakati kama Hormuz ipo katika hali ya kuzuiwa.
    wPili, aliitaka Ulaya kuelekeza nguvu zaidi katika kupunguza utegemezi ambao, kwa maneno yake, “umeilazimisha kulipia gharama za vita ambavyo si chaguo lake.”Katika mahojiano hayo yaliyofanyika saa chache kabla ya kutolewa kwa jibu la Iran kuhusu pendekezo la amani la Marekani, waziri alisema Iran—inayodai kuhitaji kuondolewa kwa vikwazo kama sehemu ya makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia—haiwezi kutarajia hatua hiyo huku hali ya usalama katika Mlango wa Hormuz ikiwa bado tete.

  • Didier Drogba Tanzania

    Didier Drogba Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mshambuliaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast na Timu ya Chelsea ya Uingereza Didier Drogba mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 05 Mei, 2026.

  • Washington Post: uharibifu uliofanywa na Iran ni mkubwa kuliko maelezo

    Washington Post: uharibifu uliofanywa na Iran ni mkubwa kuliko maelezo

    Uchambuzi wa picha za satelaiti uliofanywa na gazeti la Washington Post unaonyesha kuwa tangu kuanza kwa vita, mashambulizi ya Iran yameharibu au kuathiri angalau miundombinu na vifaa 228 katika vituo 15 vya kijeshi vya Marekani vilivyoko Mashariki ya Kati.

    Kwa mujibu wa uchambuzi huo, malengo ya mashambulizi yalijumuisha hangari za ndege, mabweni ya wanajeshi, maghala ya mafuta, ndege, mifumo ya rada, vifaa vya mawasiliano, pamoja na mifumo ya ulinzi wa anga kama Patriot na THAAD.

    Ripoti inaonyesha kuwa Bahrain na Kuwait ndizo nchi zilizoathirika zaidi, huku pia athari zikiripotiwa katika Qatar, Saudi Arabia, Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

    Kiwango cha uharibifu kilichobainishwa katika uchambuzi huu kinaelezwa kuwa kikubwa zaidi kuliko kile ambacho serikali ya Marekani imewahi kutangaza hadharani.

    Taarifa zilizotolewa hapo awali zinaonyesha kuwa wanajeshi saba wa Marekani walipoteza maisha na zaidi ya 400 kujeruhiwa katika mashambulizi hayo.Wachambuzi wanasema picha za satelaiti zinaonyesha uharibifu uliotokea katika maeneo mbalimbali ya kijeshi na zinaibua maswali kuhusu uimara wa mifumo ya ulinzi katika eneo hilo.

    Hadi sasa, Ikulu ya White House haijatoa tamko rasmi kuhusu matokeo ya uchambuzi huo.

  • Trump Aitaka Iran Kutoa Jibu la Haraka kwa Pendekezo lake la Amania

    Trump Aitaka Iran Kutoa Jibu la Haraka kwa Pendekezo lake la Amania

    Kituo cha Al-Arabiya kikinukuu chanzo cha serikali ya Pakistan kimeripoti kuwa Rais wa Marekani ameiomba Iran kutoa jibu la haraka kwa pendekezo la amani lililotumwa na Washington. Kwa mujibu wa chanzo hicho, Iran huenda ikawasilisha jibu hilo leo kupitia Serikali ya Pakistan.

    Chanzo hicho kimeeleza kuwa mawasiliano kati ya maafisa wa Pakistan na Iran bado yanaendelea bila changamoto yoyote, na kwamba hakuna kikwazo kinachozuia pande hizo mbili kuendeleza mazungumzo au kubadilishana taarifa.

    Aidha, katika mazungumzo hayo, chanzo cha Pakistani kimetaja umuhimu wa Mlango Bahari wa Hormuz na kusema kuwa suluhisho la muda mrefu kuhusu eneo hilo nyeti la kimkakati linaonekana kuwa ndani ya uwezo wa kufikiwa.

  • Rais Tshisekedi aazimia kugombea muhula wa tatu wa urais, Kongo

    Rais Tshisekedi aazimia kugombea muhula wa tatu wa urais, Kongo

    Rais Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amezungumzia uwezekano wa kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tatu, akisema atakubali kuendelea kuiongoza nchi hiyo iwapo ataungwa mkono na Wakongo kupitia kura ya maoni.Akizungumza katika mkutano na wanahabari siku ya Jumatano, Tshisekedi mwenye umri wa miaka 62 alisisitiza kuwa binafsi hakutaka kuongeza muda wake wa kukaa madarakani zaidi ya kikomo cha mihula miwili kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Kidmeokrasia ya Kongo unaomalizika mwaka wa 2028.“Sijawahi kufikia kuwania muhula wa tatu, lakini ninawaambia: Kama wananchi wa Kongo wanataka niendelee na muhula wa tatu, nitakubali,” amesema Rais wa Felix Tshisekedi.Ameongeza kuwa: Marekebisho yoyote ya Katiba yanayoruhusu hatua hiyo yatafanyika tu kwa idhini ya umma.Tshisekedi pia ametahdharisha kuwa mzozo unaoendelea mashariki mwa Kongo unaweza kupelekea kuahirishwa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika 2028.Mapigano kati ya wanajeshi wa Kongo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda yameongezeka katika majimbo yenye utajiri wa madini ya Kivu Kaskazini na Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.