Rais wa Ufaransa Macron:
“Yeyote anayeipuuza Afrika hii leo anakosea na anaupoteza mustakabali wake mwenyewe”

Mamia ya waungaji mkono wa uongozi wa serikali ya kijeshi ya Mali Jumamosi walijumuika katika uwanja wa michezo katika mji mkuu, Bamako ili kuthibitisha uungaji mkono wao kwa serikali ya mpito ya nchi hiyo.Wananchi wa Mali walijumuika mjini Bamako kufuatia wito wa serikali ya mpito ya nchi hiyo ambayo imekuwa madarakani tangu mwaka 2020 huku ikikabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo wenye silaha.Wananchi wa Mali kwa mara nyingine tena wametangaza uungaji mkono wao kwa serikali kufuatia mashambulizi yaliyoratibiwa na makundi ya waasi mwezi uliopita ambayo yalisababisha vifo vya watu kadhaa, akiwemo Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, Sadio Camara. Aprili 26 Mali ilikabiliwa na moja ya mashambulizi makubwa zaidi ya makundi yenye silaha dhidi ya jeshi la nchi hiyo katika mji mkuu, Bamako na miji mingine kadhaa.

Ripoti za kuongezeka vifo baina ya mahujaji waliokwenda Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Hija imezua wasiwasi na taharuki baina ya viongozi na wasimamizi wa ibada hiyo.Wasaudia wanasisitiza kwamba ongezeko la vifo halina uhusiano wowote na virusi, lakini sasa kwa kuwa zimesalia wiki mbili tu kabla ya kuanza ibada ya Hija, wanafikiria kuimarisha na kuongeza idadi ya timu za matibabu.Mahujaji 23 kutoka nchi nne wamefariki dunia nchini Saudi Arabia katika siku zilizotangulia kuanza msimu wa Hija wa 2026. Ikithibitisha takwimu hizo, Wizara ya Afya ya Saudi Arabia imetangaza kwamba “hali imedhibitiwa na hakuna habari za mlipuko wa virusi maalumu.”Miaka miwili iliyopita, zaidi ya mahujaji 1,300 walifariki dunia kutokana na kiharusi cha joto wakati wa ibada ya Hija kutokana na joto kali.Mwaka huu, licha ya kushuka kwa halijoto, mahujaji 10 kutoka Indonesia, 10 kutoka Bangladesh, Wairaqi wawili na mmoja wa Malaysia wamefariki dunia kutokana na kiharusi cha joto.

Falme za Kiarabu (UAE) zimeripotiwa kuwakamata na kuwafukuza maelfu ya wafanyakazi wa Pakistan muda mfupi baada ya Pakistan kusaidia kupatanisha usitishaji wa mapigano kati ya Marekani na Iran. Kulingana na ripoti, wengi wa waliokamatwa wanadaiwa kuwa Waislamu wa madhehebu ya Shia.Baadhi ya waliorejeshwa Pakistan walisema walikamatwa ghafla bila maelezo, wakashikiliwa katika mazingira magumu ya kizuizini, na akaunti zao za benki kufungwa. Walisema pia walifukuzwa haraka kutoka nchini bila kupewa sababu rasmi.Suala hili limeibua wasiwasi kwa sababu takriban Wapakistani milioni mbili wanafanya kazi katika UAE, na hutuma mabilioni ya dola kwa familia zao nchini Pakistan kupitia fedha za ughaibuni.
Chanzo: The New York Times.