Putin amesema kuwa kuendelea kwa vita kati ya Marekani na Iran hakutanufaisha upande wowote.
Amesema pia kuwa mgogoro huo ni mgumu sana na umeiweka Urusi katika hali ngumu, akieleza kwamba Moscow ina uhusiano mzuri na Iran pamoja na nchi za Kiarabu.

Trump anaripotiwa kuchoshwa na kukatishwa tamaa na vita dhidi ya Iran, huku mzozo huo ukiendelea kwa muda mrefu zaidi kuliko alivyotarajia na bila dalili ya ushindi wa wazi. Kulingana na taarifa hiyo, Trump angependa kuelekeza tena umakini wake kwenye masuala mengine, ikiwemo siasa za ndani za Marekani, mazungumzo ya biashara na China, pamoja na vipaumbele vingine vya sera.
Hata hivyo, Iran inaendelea kupinga mazungumzo na hivyo kurefusha mzozo huo.
Chanzo: The Atlantic

Rais Masoud Pezeshkian amesimulia kwa kina mkutano wake wa hivi karibuni na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Mojtaba Khamenei, akielezea hali ya kikao hicho pamoja na sifa za binafsi, kimaadili na kiuongozi alizozishuhudia kwa Kiongozi huyo.
Rais Pezeshkian amesema mkutano huo ulifanyika katika mazingira ya ukarimu na uaminifu na kuendelea kwa takriban masaa mawili na nusu.
Kwa mujibu wa Rais Pezeshkian, kilichojitokeza zaidi kuliko jambo lolote ni mtazamo wa unyenyekevu, uaminifu wa dhati na heshima ya hali ya juu wa Kiongozi Muadhamu, mwenendo uliogeuza kikao hicho kuwa majadiliano yaliyojengwa juu ya imani, utulivu, kuelewana na mazungumzo ya wazi ya moja kwa moja.
Rais Pezeshkian amesisitiza pia umuhimu wa kuimarisha mshikamano, kuaminiana na huruma katika ngazi zote za usimamizi wa serikali na utawala wa nchi.
Amebainisha kuwa pale kiongozi wa juu kabisa wa taifa anaposhirikiana na maafisa na wananchi kwa maadili ya hali ya juu, unyenyekevu na roho ya kuwajali watu, mwenendo huo huwa mfano wa kuigwa katika mfumo mzima wa utawala na uongozi wa nchi.