Mwandishi: Hussein Suleiman

  • Hofu yatanda kuhusu ushiriki wa referee Omar Artan katika kombe la dunia 2026 baada ya kuzuiwa kuingia Marekani

    Hofu yatanda kuhusu ushiriki wa referee Omar Artan katika kombe la dunia 2026 baada ya kuzuiwa kuingia Marekani

    Mwamuzi nyota kutoka Somalia, Omar Artan, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kunyimwa ruhusa ya kuingia nchini Marekani, hali ambayo imezua maswali mengi kuhusu hatma yake ya kuchezesha katika michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2026.

    Artan, ambaye ni mwamuzi mwenye beji ya FIFA tangu mwaka 2018 na ambaye hivi karibuni alitunukiwa tuzo ya Mwamuzi Bora wa Mwaka wa Wanaume wa CAF kwa mwaka 2025, alikuwa amejumuishwa kwenye orodha ya maofisa 52 waliochaguliwa kusimamia michuano hiyo mikubwa duniani.

    Kufikia sasa, sababu za kuzuiliwa kwake kuingia nchini humo hazijawekwa wazi, huku wadau wa soka wakisubiri kuona hatua zitakazochukuliwa na mamlaka husika, ikiwemo FIFA, kufuatia tukio hili linaloweza kumtoa mwamuzi huyo kwenye kinyang’anyiro cha kuchezesha katika michuano hiyo ya kihistoria.

    Tutazidi kuwapa taarifa zaidi kadiri tutakavyozidi kupata undani wa kisa hiki.

  • Mohsen Rezaee: Tuliwaonya

    Mohsen Rezaee: Tuliwaonya

    Afisa mwandamizi wa Iran;

    Mohsen Rezaee:Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikuwa imetangaza mara kwa mara kwamba haitavumilia ukiukaji wa usitishaji vita au uchokozi dhidi ya Lebanon.

    Usiku wa leo, wachokozi wamepokea jibu lao. Jibu hili ni onyo kwao kusitisha uovu wao; kila hatua mpya itakabiliwa na jibu kali zaidi na gharama nzito zaidi.

  • Chuki na mashambulizi ya chacha dhidi ya wageni Afrika Kusini

    Chuki na mashambulizi ya chacha dhidi ya wageni Afrika Kusini

    SIKU nne zilizopita, mhamiaji kutoka Msumbiji, Lado Amido, alifungua mlango wake baada ya kusikia hodi katika mji wa Kleinmond nchini Afrika Kusini.

    Alipofungua, alikutana na umati wenye hasira uliomwambia kuwa wageni kama yeye walipaswa kuondoka. Kundi hilo lilikuwa likizunguka nyumba kwa nyumba likitoa ujumbe huo huo.

    Amido alikimbia na kujificha milimani kwa siku mbili. Sasa anaishi katika ukumbi wa mji huo pamoja na wahamiaji wengine kutoka Malawi na Msumbiji katika Mkoa wa Western Cape.

    Wote wamelazimika kujificha kutokana na makundi yenye chuki dhidi ya wageni yaliyoshambulia miji kadhaa ya maeneo ya pwani.

    Kisa chake kinaonyesha tu jinsi Afrika Kusini inaendelea kukumbwa na wimbi la maandamano dhidi ya wahamiaji.

    Kutokana na hatari iliyoko, serikali ya Msumbiji ilisema raia wake watano waliuawa katika mji wa Mossel Bay.

    Amido anaishi Kleinmond, takriban kilomita 300 kutoka Mossel Bay.

    “Mei 31, watu walifika nyumbani kwangu, wakagonga mlango na kisha wakachukua mali yangu yote,” akasema Amido, 49.

    Amekuwa Afrika Kusini tangu Februari baada ya kuwasili nchini humo kutafuta kazi.

    Katika ukumbi wa mji wa Kleinmond, anaishi pamoja na takriban wahamiaji 100 wengine, baadhi yao wakitarajia kurejea makwao.

  • Kenya kuanza kuzoa mapato ya mafuta Ghafi ya Turkana

    Kenya kuanza kuzoa mapato ya mafuta Ghafi ya Turkana

    AFUENI KWA KENYA BAADA YA KUANZA kuzalisha mafuta kabla ya mwisho wa mwaka huu kutoka kaunti ya Turkana kaskazini mwa nchi.

    Waziri wa Kawi na Mafuta Opiyo Wandayi hivyo Ijumaa Juni 5, 2026 alifafanua kuwa ni mafuta ghafi yatakayozalishwa na kuuzwa ng’ambo kusafishwa kutoa petroli, dizeli na bidhaa nyininezo.

    “Kabla ya mwisho wa mwaka huu tutaanza kuzalisha mafuta kutoka Turkana. Baada ya muda mrefu hatimaye utekelezaji wa mradi huu umepiga hatua hadi kufikia kiwango cha uzalishaji,” akaeleza kwenye mahojiano katika Radio Jambo, akiutaja mradi huo kama yenye umuhimu mkubwa katika sekta ya kawi.

    “Mafuta ghafi kutoka Turkana yatauzwa ng’ambo kwa sababu wakati huu hatuma kiwanda cha kusafisha mafuta. Mapato kutkana na uuzaji wa mafuta hayo yatafaidi Wakenya wote sio tu wakazi wa Turkana,” Bw Wandayi akaeleza.

    Mwezi jana, Rais William Ruto alifichua mpango wa kuanzishwa kwa kiwanda cha kusafisha mafuta katika ukanda wa Afrika Mashariki, kwa ushirikiano na bwanyenye wa Nigeria Aliko Dangote.

    Alisema kuwa kampuni hiyo itaanzishwa eneo la Tanga, nchini Tanzania.

    Kampuni ya Gulf Energy Ltd ndio itakuwa ikichimba mafuta kutoka visima vilivyoko Lokichar, eneo bunge la Turkana Kusini.

    Kampuni hiyo ilitwaa usimamizi wa mradi huo baada ya kutwaa shughuli ya mali ya kampuni ya Tullow Oil, ya Uingereza, iliyoanzisha uchimbaji wa mafuta eneo hilo miaka 10 iliyopita.

    Wakati huu Kenya hununua mafuta yaliyosafishwa kutoka ukanda wa Mashariki ya Kati, linaloshuhudia vita kati ya Amerika na Iran.

    Vita hivyo vilivyoanza Februari 28, vimevuruga usafirishaji wa bidhaa hiyo kupitia Mkondo wa Hormuz, hali ambayo imechangia kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

    Hata hivyo, mapema wiki huu Waziri Wandayi alielezea matumaini  kuwa bei ya mafuta itashuka hivi karibuni, baada ya serikali kuanza kupata mafuta kwingineko, hali itakayoleta afueni kwa Wakenya

  • Katz: “Hakuna Kusitisha Mapigano Nchini Lebanon

    Katz: “Hakuna Kusitisha Mapigano Nchini Lebanon

    “Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, ametoa tamko zito kuhusu hali ya usalama nchini Lebanon, akisisitiza kuwa hakuna makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano yanayoendelea katika eneo hilo.

    Katika taarifa yake, Waziri Katz ameweka bayana kuwa jeshi la Israel litaendelea na operesheni zake dhidi ya ‘kundi la Wapinzani’ bila kupumzika.

    Tamko hili linakuja kinyume na taarifa za awali ambazo zilikuwa zikidokeza kuwa huenda kukawa na kulegeza kamba au kupungua kwa mvutano katika mpaka wa Israel na Lebanon kufuatia mazungumzo ya kidiplomasia.

    Hadi sasa, hali inasalia kuwa tete huku jeshi la Israel likionekana kuongeza kasi ya mashambulio yake, hatua ambayo wachambuzi wanaiita kuwa ni ishara ya kuendeleza msukumo wa kijeshi licha ya shinikizo la kimataifa la kutafuta amani.

  • Waziri wa hazina wa Marekani kupitia Fox News: Nini Maana ya ‘Kumaliza Kazi’

    Waziri wa hazina wa Marekani kupitia Fox News: Nini Maana ya ‘Kumaliza Kazi’

    Waziri wa Hazina wa Marekani amesema katika mahojiano na Fox News kwamba Marekani inaweka mbele masuala matatu kama kigezo cha “kumaliza kazi” katika mazungumzo yanayohusiana na Iran, huku akirudia madai ya Washington dhidi ya Tehran.

    Katika kauli yake, Waziri huyo alidai kuwa “kumaliza kazi” kunamaanisha kuhakikisha Mlango-Bahari wa Hormuz unabaki wazi, kuchukua urani iliyorutubishwa kwa kiwango cha juu, na kuhakikisha Iran haina silaha ya nyuklia.

    Wakati huohuo, Iran imesisitiza haki yake ya mamlaka juu ya Mlango-Bahari wa Hormuz na imeeleza kupinga kwake wazo la kukabidhi Marekani urani yenye kiwango cha juu cha urutubishaji.

    Kauli hizi zinatolewa huku vyombo vya habari vya Marekani, CNN na CBS, vikiripoti hapo awali kuhusu kile walichokitaja kuwa ni matakwa makubwa ya Donald Trump katika duru ya mwisho ya mazungumzo kupitia wapatanishi, pamoja na “mabadiliko makubwa” yanayodaiwa kuingizwa kwenye maandishi ya hati ya maelewano.