Mwandishi: Suleiman Ali

  • Mwakilishi wa Bunge la Marekani asema Trump ni tishio kwa usalama wa nchi

    Mwakilishi wa Bunge la Marekani asema Trump ni tishio kwa usalama wa nchi

    Mwakilishi wa Chama cha Democratic katika Bunge la Marekani, Seth Moulton, amesema kuwa rais wa Marekani Donald Trump ni tishio kwa usalama na uthabiti wa Marekani.

    Akizungumza kuhusu wasiwasi unaoibuka juu ya umri na mwenendo wa Trump, Moulton alisema ni kawaida kwa watu wanapozeeka kupungua uwezo wao wa kufanya maamuzi, lakini hali hiyo inaweza kuwa hatari zaidi inapomhusu mtu anayewania au kushika nafasi muhimu ya uongozi wa taifa.

    Moulton alisisitiza kuwa, kwa maoni yake, wananchi wengi wanaona Trump kuwa hatari kwa wanajeshi wa Marekani, uchumi wa nchi pamoja na usalama wa taifa.

    wAliongeza kuwa orodha ya masuala yanayozua wasiwasi kuhusu Trump ni ndefu, akisema pia kwamba kwa sasa Trump anaonekana kuwa hatari zaidi kuliko alivyokuwa wakati wa muhula wake wa kwanza wa urais.

  • Ehud Barak: Netanyahu Amekuwa Kikaragosi cha Trump

    Ehud Barak: Netanyahu Amekuwa Kikaragosi cha Trump

    Waziri mkuu wa zamani wa Israel, Ehud Barak, amekosoa vikali mwenendo wa Waziri Mkuu wa sasa, Benjamin Netanyahu, katika mahusiano yake na Marekani.

    Katika kauli yake, Barak alisema kuwa Netanyahu amegeuka kuwa “kikaragosi mikononi mwa Donald Trump,” akionyesha wasiwasi kuhusu namna serikali ya Israel inavyoendesha uhusiano wake na Washington.

  • Mufti wa Oman awataka Waislamu kuunga mkono Iran na Gaza

    Mufti wa Oman awataka Waislamu kuunga mkono Iran na Gaza

    Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmed Al‑Khalili, ametoa wito kwa Waislamu duniani kuonyesha mshikamano wao na Iran na Gaza kufuatia maendeleo ya hivi karibuni katika eneo la Mashariki ya Kati.

    Katika kauli yake kuhusu hali ya eneo hilo, Sheikh Al‑Khalili alisisitiza umuhimu wa umoja wa ulimwengu wa Kiislamu mbele ya mashambulizi yanayolenga nchi na maeneo ya Kiislamu.

    Amesema Waislamu wanapaswa kusimama pamoja na kuonyesha mshikamano dhidi ya aina yoyote ya uchokozi unaolenga Gaza, Iran au sehemu nyingine za ardhi za Kiislamu.

    Mufti huyo pia alisisitiza kuwa Umma wa Kiislamu ni umma mmoja, na kwamba umoja na mshikamano ni muhimu katika kukabiliana na changamoto na mashambulizi dhidi ya nchi za Kiislamu.

  • Maandamano Dhidi ya Netanyahu: Vyombo vya Dola Vyaingilia Kati Kudhibiti Umati Tel Aviv na Jerusalem

    Maandamano Dhidi ya Netanyahu: Vyombo vya Dola Vyaingilia Kati Kudhibiti Umati Tel Aviv na Jerusalem

    Taarifa kutoka katika vyombo vya habari zinaonyesha kuwa mamia ya waandamanaji walijitokeza barabarani wakipinga serikali ya Netanyahu, huku vikosi vya usalama vikisimamisha magari ya kupambana na ghasia pamoja na kutumia magari ya kunyunyizia maji kwa ajili ya kuwatawanya.

    Katika jiji la Tel Aviv, waandamanaji walikusanyika katika Uwanja wa Habima wakimtuhumu waziri mkuu huyo na baraza lake la mawaziri kwa, kwa madai yao, kushindwa kukabiliana na kundi la Hamas.

    Wakati huohuo, mjini Jerusalem inayokaliwa kimabavu, idadi kubwa ya watu ilishiriki maandamano hayo, na kusababisha polisi kuingilia kati kwa kutumia magari ya maji ili kudhibiti umati.

    Hadi sasa, hakuna taarifa za majeruhi zilizotolewa, lakini hali ya taharuki imeendelea kushuhudiwa katika maeneo hayo.

  • Kampuni ya Trump Media Yaripoti Hasara ya Zaidi ya Dola Milioni 400

    Kampuni ya Trump Media Yaripoti Hasara ya Zaidi ya Dola Milioni 400

    Kampuni ya Trump Media and Technology Group, mmiliki wa jukwaa la Truth Social lililoanzishwa na Rais wa Marekani Donald Trump, imeripoti hasara halisi inayozidi dola milioni 400 katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

    Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, hasara hiyo imetokana na kuporomoka kwa soko la sarafu za kidijitali, hususan Bitcoin, ambalo limeathiri kwa kiasi kikubwa thamani ya uwekezaji wake.

    Mwaka mmoja uliopita, kampuni hiyo ilitangaza kukusanya dola bilioni 2.5 kwa lengo la kuwekeza katika sekta ya sarafu za kidijitali, ambayo imekuwa miongoni mwa maeneo yenye kipaumbele kwa Rais Trump katika masuala ya biashara na teknolojia.

  • Onyo Kali la Iran: Tutapiga Kambi na Meli za  Marekani Ikiwa Meli Zetu Zitashambuliwa

    Onyo Kali la Iran: Tutapiga Kambi na Meli za Marekani Ikiwa Meli Zetu Zitashambuliwa

    Jeshi la Wanamaji la Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) nchini Iran limetoa onyo kwamba shambulio lolote dhidi ya meli zake za mafuta au meli za kibiashara litajibiwa kwa kulenga kambi za Marekani pamoja na vifaa vyake vya kijeshi vya majini katika eneo hilo. Taarifa hiyo imeripotiwa na vyombo vya habari vya serikali ya Iran.