Mwandishi: Suleiman Ali

  • Mgombea urais wa Ufaransa Mélenchon Aishutumu Israel, Asema Ni Tishio Kubwa Zaidi Mashariki ya Kati

    Mgombea urais wa Ufaransa Mélenchon Aishutumu Israel, Asema Ni Tishio Kubwa Zaidi Mashariki ya Kati

    Jean-Luc Mélenchon, mgombea wa urais wa Ufaransa, amesema kuwa Israel kwa sasa ndiyo nchi hatari zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.

    Ameieleza Israel kuwa ndiyo inayowashambulia majirani zake, kuchochea vita, na kutekeleza mauaji ya kimbari, akibainisha kuwa anapoitaja Israel analenga serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

    Katika kauli nyingine, Mélenchon amesema aliwahi kumuuliza jenerali anayesimamia kikosi cha Umoja wa Mataifa kuhusu hatua ambazo zingechukuliwa iwapo Netanyahu angeivamia Lebanon. Kwa mujibu wa Mélenchon, jenerali huyo alimjibu kuwa maagizo yao ni kujiondoa.

    Mélenchon amesema hakuelewa namna kikosi cha kulinda amani kinaweza kujiondoa badala ya kuingilia kati ili kuzuia mapigano.Aidha, amesema kuwa iwapo askari wa Ufaransa atashambuliwa, basi Ufaransa inapaswa kujibu.

    Pia amesisitiza kuwa ndege za Marekani hazipaswi kuruka juu ya anga ya Ufaransa wala kutumia kambi za kijeshi za Ufaransa, akieleza wazi kuwa anapinga hali hiyo.

  • Wall Street Journal: Iran yaibananga Marekani katika Vita vya Masimulizi

    Wall Street Journal: Iran yaibananga Marekani katika Vita vya Masimulizi

    Gazeti la Wall Street Journal limeripoti kuwa Iran inaendelea kupata nguvu katika vita vya taarifa kupitia uzalishaji na usambazaji wa video kadhaa zilizotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili bandia (AI).

    Kwa mujibu wa gazeti hilo, video hizo zimeenea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na zimekuwa sehemu ya mkakati wa kuongeza ushawishi katika majukwaa ya kimataifa.

    Ripoti hiyo inaeleza kuwa lengo kuu la video hizo ni kuchochea mgawanyiko wa kisiasa ndani ya Marekani. Imebainishwa kuwa klipu hizo hutayarishwa na kusambazwa na makundi yanayoiunga mkono Iran pamoja na baadhi ya ofisi za kidiplomasia za nchi hiyo.

    Mara nyingi video hizo huonesha kwa kejeli hatua na mikakati ya kijeshi ya Marekani. Katika moja ya video zilizotajwa kwenye ripoti, rais wa Marekani, Donald Trump, ameonyeshwa kwa sura ya mharamia katika mandhari yanayofanana na filamu Pirates of the Caribbean.

    Video hiyo inaonyesha majeshi ya Marekani yakijaribu kufungua tena Mlango wa Bahari wa Hormuz na kuizingira bandari za Iran, lakini juhudi hizo zikimalizika kwa kushindwa huku meli za Marekani zikiharibiwa.

  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar ajadili na JD Vance kupunguza mvutano Mashariki ya Kati

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar ajadili na JD Vance kupunguza mvutano Mashariki ya Kati

    Washington — Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amekutana na Makamu wa Rais wa Marekani, J.D. Vance, mjini Washington kujadili juhudi za kupunguza mvutano katika eneo.

    Katika mazungumzo hayo, pande hizo zilijadili umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa wahusika mbalimbali ili kupunguza mivutano na kuimarisha utulivu wa kikanda.

    Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar alisisitiza pia umuhimu wa kuendelea na juhudi za upatanishi, ikiwemo nafasi ya Pakistan katika kuleta pande husika karibu, pamoja na haja ya kufikiwa kwa makubaliano ya kina yatakayosaidia kufanikisha amani ya kudumu katika eneo hilo.

  • Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Iran sasa ina nguvu ya kushinikiza

    Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Iran sasa ina nguvu ya kushinikiza

    Antony Blinken, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, amesema kuwa hali ya sasa inaonyesha kuwa Iran imepata nafasi ya kutumia nguvu ya ushawishi katika mwelekeo wa mazungumzo na hatua zinazoweza kufuata.

    wKwa mujibu wa Blinken, Donald Trump anatafuta njia ya kujinasua, huku akieleza matumaini yake kwamba makubaliano yatafikiwa.

    Aidha, aliongeza kuwa Iran sasa inashikilia nyenzo ya shinikizo na inatarajiwa kuitumia kwa manufaa yake katika hatua zijazo.

  • Urusi na China kupinga azimio la Marekani la Hormuz dhidi ya Iran katika umoja wa mataifa

    Urusi na China kupinga azimio la Marekani la Hormuz dhidi ya Iran katika umoja wa mataifa

    Urusi na China zinatarajiwa kupiga kura ya turufu dhidi ya rasimu ya azimio lililowasilishwa na Bahrain na Marekani kuhusu hali ya usalama katika Mlango wa Hormuz, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya kimataifa.

    WMtandao wa Al Jazeera umearifu kuwa hadi sasa Moscow na Beijing hawajawasilisha mapendekezo yoyote ya marekebisho kwa rasimu hiyo.Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa rasimu iliyowasilishwa na Marekani na Bahrain inaonekana kufanana kwa kiasi kikubwa na ile ambayo awali ilikataliwa na Urusi na China.

  • CBS: Mashambulizi mapya dhidi ya meli za kivita za Marekani yalikuwa makali zaidi kuliko yale ya siku chache zilizopita

    CBS: Mashambulizi mapya dhidi ya meli za kivita za Marekani yalikuwa makali zaidi kuliko yale ya siku chache zilizopita

    Washington, Marekani — Vyanzo vya shirika la habari la CBS vimeripoti kuwa meli za kivita za Marekani, USS Truxtun na USS Mason, zimeshambuliwa vikali na vikosi vya Iran katika Bahari ya Oman.

    Maafisa wa Marekani wameeleza kuwa mashambulizi hayo yalikuwa makubwa na ya muda mrefu zaidi ikilinganishwa na yale yaliyotekea siku kadhaa zilizopita.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, boti za kasi za Iran zilikaribia manowari hizo kwa umbali hatari, hali iliyozilazimisha meli za Marekani kutumia mizinga ya baharini, mfumo wa silaha za kujihami za karibu (CIWS) pamoja na bunduki zilizowekwa juu ya staha.

    AAidha, maafisa wa Marekani wamesema kuwa Iran ilitumia ndege zisizo na rubani (drones) na makombora katika oparesheni hiyo, jambo lililoonyesha ongezeko la uhasama na hatari katika eneo la ghuba.