Lebo: Hormuz

  • Baada ya onyo la Iran, Macron akana mpango wa kupeleka meli za kivita Hormuz

    Baada ya onyo la Iran, Macron akana mpango wa kupeleka meli za kivita Hormuz

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuwa nchi yake haikuwahi kupanga kupeleka vikosi vya majini katika Mlango wa Hormuz.

    Badala yake, amesema Ufaransa ilikuwa inapendekeza ujumbe wa usalama wa kidiplomasia ambao ungefanyika kwa uratibu na Iran.Akizungumza kuhusu hali ya usalama katika eneo hilo, Macron alisisitiza kuwa operesheni za kijeshi za kutumia nguvu kufungua tena mlango huo wa bahari si jambo linalowezekana na zinaweza kuongeza hatari wakati mvutano wa kikanda ukiendelea.

    Kwa mujibu wa rais huyo, hatua ya kwanza inapaswa kuwa kusitishwa kwa mapigano, kisha kufanyika mazungumzo ya kimataifa yanayohusisha Iran ili kuhakikisha usafiri wa baharini unakuwa salama.

    Mlango wa Hormuz umeathiriwa sana tangu mwishoni mwa Februari 2026 kufuatia mashambulizi na vitisho vinavyohusishwa na uvamizi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran. Ufaransa pamoja na Uingereza zimekuwa zikishinikiza kuanzishwa kwa ujumbe wa ulinzi wa kimataifa utakaotekelezwa baada ya kupungua kwa uhasama, ukihusisha zaidi ya nchi 50 na kutenganishwa na operesheni za kijeshi za vita.

    Katika hatua nyingine, Ufaransa ilipeleka kundi la meli za kivita linaloongozwa na meli ya kubeba ndege ya Charles de Gaullekuelekea Bahari Nyekundu mapema Mei 2026 kama sehemu ya mkakati wa kuimarisha usalama bila kuongeza mvutano. Macron pia anatarajiwa kufanya mikutano na washirika kadhaa, wakiwemo India, ili kujadili uwezekano wa mfumo wa kusindikiza meli kwa hiari mara tu mashambulizi yatakapositishwa.

  • Meli ya gesi ya Qatar yaripotiwa kupita Mlango wa Hormuz kwa ruhusa ya Iran

    Meli ya gesi ya Qatar yaripotiwa kupita Mlango wa Hormuz kwa ruhusa ya Iran

    Meli ya kubeba gesi asilia iliyoyeyushwa (LNG) inayomilikiwa na Qatar, iitwayo “Al‑Khariyat”, imetuma ishara katika maji ya Bahari ya Oman, kulingana na taarifa za ufuatiliaji wa meli.

    Taarifa zinaonyesha kuwa meli hiyo ilionekana jana katika eneo la lango la Mlango wa Hormuz kabla ya kuzima mfumo wake wa utambuzi wa kiotomatiki wa meli (AIS).Meli hiyo inaripotiwa kuelekea Pakistan.

    Vyanzo vinaeleza kuwa huenda ikawa meli ya kwanza isiyohusiana na Iran kuruhusiwa kupita katika Mlango wa Hormuz na Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu tangu kuanza kwa kile kinachotajwa kama mzingiro au vitendo vya uharamia wa baharini vinavyohusishwa na Marekani.

  • Urusi na China kupinga azimio la Marekani la Hormuz dhidi ya Iran katika umoja wa mataifa

    Urusi na China kupinga azimio la Marekani la Hormuz dhidi ya Iran katika umoja wa mataifa

    Urusi na China zinatarajiwa kupiga kura ya turufu dhidi ya rasimu ya azimio lililowasilishwa na Bahrain na Marekani kuhusu hali ya usalama katika Mlango wa Hormuz, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya kimataifa.

    WMtandao wa Al Jazeera umearifu kuwa hadi sasa Moscow na Beijing hawajawasilisha mapendekezo yoyote ya marekebisho kwa rasimu hiyo.Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa rasimu iliyowasilishwa na Marekani na Bahrain inaonekana kufanana kwa kiasi kikubwa na ile ambayo awali ilikataliwa na Urusi na China.

  • Rais wa Ufaransa atafuta ushirikiano na Iran kuimarisha usalama Hormuz

    Rais wa Ufaransa atafuta ushirikiano na Iran kuimarisha usalama Hormuz

    Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ametangaza kuwa nchi yake imejitolea kikamilifu kuhakikisha usalama na utulivu wa usafiri wa baharini katika Mlango-Bahari wa Hormuz unarejea katika hali ya kawaida.

    Akizungumza juu ya umuhimu wa njia hiyo ya kimataifa, Rais Macron amesisitiza kuwa Ufaransa itafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa shughuli za usafirishaji na biashara hazivurugiki na zinaendelea kama ilivyokuwa awali.“Tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha kwamba usafiri katika Mlango-Bahari wa Hormuz unarejea katika hali ya kawaida,” alisema kiongozi huyo.

    Aidha, katika hatua ya kutafuta suluhu ya kidiplomasia, Rais Macron amebainisha kuwa anakusudia kuanza tena mazungumzo rasmi na viongozi wa Iran. Hatua hiyo inalenga kuratibu juhudi za pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kikanda ili kuzuia mivutano zaidi katika eneo hilo muhimu la kimkakati.