Mwandishi: Suleiman Ali

  • “Kwa Nini Mataifa ya Nje Yaingilie Mlango wa Hormuz?” – Mélenchon Aibua Mjadala Kuhusu Haki ya Iran Kujilinda

    “Kwa Nini Mataifa ya Nje Yaingilie Mlango wa Hormuz?” – Mélenchon Aibua Mjadala Kuhusu Haki ya Iran Kujilinda

    Mgombea wa urais wa Ufaransa Jean‑Luc Mélenchon ametoa maoni yake kuhusu Iran na Mlango wa Hormuz. Mélenchon alisema kuwa nchi inapojilinda ina haki ya kutumia mbinu mbalimbali za ulinzi. Alisema kuwa katika hali kama hiyo, mataifa mengine pia yangefanya vivyo hivyo kulinda maslahi yao ya kitaifa.

    Akizungumzia suala la Mlango wa Hormuz, alihoji sababu za mataifa ya nje kuingilia eneo hilo, akisema kuwa liko ndani ya mazingira ya kijiografia ya Iran.

    Kwa mtazamo wake, Iran haikukurupuka kuufunga mlango huo wa bahari, bali ni baada ya kukakabiliwa na uvamizi kutoka Marekani na Israel.

  • “Mwisho wa Karne ya Marekani”: Mgombea urais Ufaransa Atabiri Kuanguka kwa Utawala wa Dola

    “Mwisho wa Karne ya Marekani”: Mgombea urais Ufaransa Atabiri Kuanguka kwa Utawala wa Dola

    Mgombea wa urais wa Ufaransa Jean‑Luc Mélenchon amesema kuwa migogoro ya sasa ya kimataifa inaweza kuashiria mwisho wa kile alichokiita “karne ya Marekani”.

    wAkizungumzia nafasi ya Marekani katika mfumo wa kimataifa, Mélenchon alisema kuwa nguvu ya Marekani haitokani sana na uwezo wake wa kijeshi bali na nafasi ya dola ya Marekani katika uchumi wa dunia. Kwa mujibu wake, dola ndiyo msingi mkuu wa ushawishi wa Marekani.

    Aliongeza kuwa Marekani imejizatiti kijeshi ili kuhakikisha kuwa dola inaendelea kuwa sarafu yenye nguvu katika biashara ya kimataifa. Hata hivyo, alisema kuwa polepole baadhi ya benki kuu duniani zinaanza kupunguza utegemezi wao kwa sarafu hiyo.

  • Hofu ya Udukuzi: Ujumbe wa Marekani Watupa Zawadi za China Jalalani Kabla ya Kupanda Air Force One

    Hofu ya Udukuzi: Ujumbe wa Marekani Watupa Zawadi za China Jalalani Kabla ya Kupanda Air Force One

    BEIJING: Katika kile kinachoonekana kama hatua kali za kiusalama, wajumbe wa Marekani wameripotiwa kutupa zawadi zote walizopewa na wenyeji wao nchini China kabla ya kupanda ndege ya Rais, Air Force One.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwandishi wa gazeti la New York Post, wajumbe hao walionekana wakitupa nishani, pini na vitu mbalimbali vya ukumbusho kwenye mapipa ya taka uwanjani hapo kabla ya kuanza safari ya kuondoka jijini Beijing.

    Ripoti hiyo inafafanua zaidi kuwa, uamuzi huo ulitokana na agizo maalum la kutoruhusu kifaa chochote chenye asili ya China kuingizwa ndani ya ndege hiyo kwa hofu ya udukuzi.

    Katika kuimarisha usalama huo wa kimtandao, wajumbe hao hawakuruhusiwa kusafiri na simu zao binafsi wakati wa ziara hiyo. Badala yake, walipatiwa simu maalum zilizokuwa zimesafishwa taarifa zote na ambazo zilidhibitiwa kiusalama.

  • Ushirikiano kati ya Iran na China wazidi kuimarika licha ya safari ya Trump

    Ushirikiano kati ya Iran na China wazidi kuimarika licha ya safari ya Trump

    Ushirikiano kati ya Iran na China umeendelea kuimarika huku mataifa hayo mawili yakikabili mazingira ya migogoro katika eneo na changamoto za kimataifa.

    Wachambuzi wanaueleza mwenendo huu kama chanya na unaotarajiwa kuendelea katika kipindi kijacho.Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Seyed Abbas Araghchi, alifanya ziara rasmi mjini Beijing na kukutana na mwenzake wa China.

    Katika mazungumzo hayo, Araghchi alieleza kuwa Iran ina imani na jukumu la China katika kusaidia juhudi za kuleta utulivu, kuendeleza amani na kushughulikia mipango ya kipindi cha baada ya vita katika eneo hilo.

    Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa China alisisitiza umuhimu wa kusitishwa kabisa kwa mapigano na kuendelezwa kwa mawasiliano ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili. Alisema kuwa eneo hilo linapitia hatua nyeti, na ushirikiano wa karibu kati ya Tehran na Beijing unaweza kuwa na mchango mkubwa katika mwelekeo wa matukio.

  • Mwanadiplomasia wa Zamani wa Marekani: “Wairani Hawawezi Kusalimishwa kwa Mabomu”

    Mwanadiplomasia wa Zamani wa Marekani: “Wairani Hawawezi Kusalimishwa kwa Mabomu”

    Mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani, Ryan Crocker, ameikosoa kauli ya rais wa Marekani Donald Trump kuhusu “Iran kujisalimisha,” akiiita kauli hiyo kuwa ya kuchekesha.

    Crocker, ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani katika nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati na kushiriki katika duru kadhaa za mazungumzo na Iran, alisema kuwa Wairani ni watu wenye msimamo thabiti na uzoefu mkubwa wa vita.Kwa mujibu wa Crocker, karibu kila familia nchini Iran imeguswa kwa namna fulani na Vita vya Iran na Iraq, jambo ambalo limeifanya jamii hiyo kuwa sugu dhidi ya vitisho vya kijeshi.

    Alisisitiza kuwa ni makosa kuamini kwamba mashambulizi ya mabomu yanaweza kuwalazimisha Wairani kujisalimisha au kubadili msimamo wao wa kisiasa.